Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Kitila Mkumbo amekagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara. 


Akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani humo Januari 2, 2025, Mhe. Prof. Mkumbo amezindua na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi Wodi za Kinamama, Watoto na Wanaume katika Hospitali ya Halimashauri ya Wilaya ya Mbulu inayojengwa kwa gharama ya zaidi ya bilioni 4.

Aidha, amezindua mradi wa Ujenzi wa Mabweni na Matundu ya vyoo katika shule ya Sekondari Kainam ambapo zaidi ya shilingi milioni 400 zimetuka, na kuongeza idadi ya wanafaunzi kutoka 44 hadi kufikia 612.

Vile vile, amezindua na kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa Umeme wa Silaloda Wilayani Mbulu, ulioghalimu zaidi ya shilingi milioni 140 na kuwezesha wananchi wanaoishi Silaloda na maeneo ya jirani kupata nishati ya umeme.

Baadaye Mhe. Waziri amehitimisha ziara yake kwa siku ya kwanza kwa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara kiwango cha rami katika mji mdogo wa Hydom-Dongobeshi unaogharimu milioni 400.74 ikiwa ni fedha za mfuko wa jimbo na umefikia asilimia 70 za utekelezaji.

Akihutubia wanchi waliyojitokeza, Mhe. Waziri Prof. Mkumbo amewaka wazi kuridhishwa kwake na utekelezaji miradi hiyo katika Wilaya ya Mbulu na kusema kuwa unakwenda sambamba na malengo ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha inawafikishia wananchi huduma za kijamii ili kuboresha maisha na kuchochea shughuli za maendeleo.

Hii ni ziara ya kwanza ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo kwa mwaka 2025 ambapo ataifanya kwa siku tatu ikiwa na lengo la kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika mkoa huo kwa maagizo ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Share To:

Post A Comment: