Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ametembelea Mahabusu ya Watoto Mbeya na kutoa msaada wa chakula ikiwa ni zawadi yake ya mwaka mpya.
Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka wazazi kuwa karibu na malezi ya watoto ili kujenga Taifa bora kwani baadhi ya wazazi na walezi wameelekeza malezi kwa watoto wa kike pekee na kuwaacha watoto wa kiume.
Aidha amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyoboresha mazingira ya mahabusu za watoto nchini.
Kwa upande wake Neema Ngowi Afisa Ustawi wa Jamii ambaye pia ni Meneja Msaidizi wa Mahabusu hiyo amesema wazazi waelekeze malezi mazuri hasa kwa watoto wa kiume kwani ndiyo tunu ya Taifa watoto wasipolelewa vizuri kuna hatari ya kupoteza kizazi cha Taifa.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Salumu Manyendi mbali ya kumshukuru Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuomba kuendelea kusaidia wahitaji kikiwemo Kituo hicho.
Pia ameendelea kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia wahitaji kila sikukuu.
Post A Comment: