Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuagiza mkandarasi anayeshughulikia mnara wa mawasiliano Kijiji cha Sota Kata ya Igalula Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza kurekebisha haraka upatikanaji wa mawasiliano ya uhakika.

Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa agizo hilo katika muendelezo wa ziara yake nchini ya kutembelea minara 758 nchini fedha zilizogharamiwa na Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kukuza uchumi na kurahisisha upatikanaji wa mawasilano ya kidijitali.

Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema Serikali imeendelea kuboresha mkongo wa Taifa kwa kurahisisha mawasilano na kuongeza mapato ya TTCL na Serikali kwa ujumla.

Awali Wilaya ya Sengerema ilikuwa ina changamoto ya upatikanaji wa mawasilano ya uhakika ambapo mnara huo umegharimu shilingi 135m.

Mwakilishi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF) Edward Rutaboba amesema kukamilika kwa mnara huo kutanufaisha wananchi zaidi ya elfu ishirini na sita katika Kata hiyo.






Share To:

Post A Comment: