Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa amechangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana Sekondari ya wasichana Kata ya Shuzuvi Wilaya ya Mbeya.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka wazazi kuwa karibu katika malezi ya watoto wa kiume kwani wasisite kuwakagua ili wawe na kesho iliyo njema.

Aidha amewataka wananchi wa Shizuvi kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na kufanya maendeleo makubwa katika elimu, barabara,maji na nishati huku akiahidi kuendelea kuwatumia kwa uadilifu na kuwaletea shida za wanawake.

Diwani wa Kata ya Shizuvi Noah Mwashibanda amemshukuru Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kufika Shizuvi na kusikiliza changamoto zao ikiwemo ya barabara na ujenzi wa bweni la wasichana.

Subira Mwangoka ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mbeya ameunga mkono kwa Jumuia yake kuchangia shilingi laki tano.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Gideon Mapunda amechangisha papo hapo shilingi laki tatu na elfu hamsini ambapo Halmashauri itamalizia bweni hilo.













Share To:

Post A Comment: