Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara leo terehe 14 Januari, 2025 amemuwakilisha Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama kuwasilisha taarifa kuhusu mipango na mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya dharura nchini mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma, Wizara imewasilisha mkakati wake wa kukabiliana na magonjwa ya dharura na mlipuko ikiwemo kuanzisha vituo vya operesheni za matukio ya dharura.

Wasilisho hilo pia lilihusisha kufanya tathmini ya matukio ya dharura na magonjwa ya mlipuko, kutoa mafunzo kwa watoa huduma ikiwemo wahudumu wa afya ngazi ya jamii (CHWs), kuimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa kinga, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na kuchakata taarifa za matukio husika katika mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa katika jamii.











Share To:

Post A Comment: