Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka watoa huduma za mawasilano nchini kuacha binafsi badala yake wawe wazalendo washirikiane ili wananchi wapate mawasilano badala ya kila mmoja kusimika mnara wake lengo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita.

Ameyasema hayo Kisiwa cha Ukara Wilaya ya Ukerewe Mkoa wa Mwanza ikiwa ni mfululizo wa kutembelea na kukagua minara 758 nchini katika mradi unaosimamiwa na serikali ukiwa ni mpango mahsusi wa kuboresha mawasiliano kidijitali kitaifa na Kimataifa.

Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema Serikali kwa sasa imeongeza nguvu kuhakikisha kila eneo linafikiwa na mkongo wa Taifa wa mawasiliano ili kuboresha huduma kidijitali.

Aidha ameitaka Kampuni ya Halotel kufanya maboresho ya mnara huo ili sasa wananchi waanze kutumia simu janja.

Mwakilishi wa mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF) Kanda ya Ziwa Mhandisi Edward Benedict Rutaboba amesema mradi huo ni miongoni mwa miradi nane inayotekelezwa Mkoani Mwanza ikiwa ni awamu ya pili na amemhakukishia Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuwa Wilaya ya Ukerewe inatekeleza miradi miwili.

Joseph Juma Nyamasaba mkazi wa Ukerewe ameipongeza Serikali kwa kutekeleza mdadi huo kwani unewarahisishia upatikanaji wa mawasilano tofauti na awali ambapo walikuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta mawasilano ya simu.











Share To:

Post A Comment: