Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Hamidu Aweso (Mb.), amewaasa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuacha kuzoea shida za wananchi, na badala yake kuzitafutia ufumbuzi ili wananchi wapate huduma ya Majisafi ya uhakika.
Waziri Aweso amewaasa Wafanyakazi hao wakati wa Mkutano Maalum wa Tatu Baraza la Saba la Wafanyakazi wa DUWASA lililofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Tume ya Maadili, ambalo pamoja na mambo mengine limepitia Rasimu ya Bajeti ya Mamlaka hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026
Aidha, Mhe. Aweso amesema, wananchi watapata huduma bora iwapo Wafanyakazi na Menejimenti watafanya kazi na kutekeleza wajibu wao kwa ushirikiano, kusikilizana, na kuepuka upendeleo ambao huzaa manung'uniko mahali pa kazi na kushusha ufanisi.
"Muwe na Utamaduni wa Kuneneana Mema" - alisisitiza
Ameitaka DUWASA kuendelea kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa Miradi mikubwa ya Majisafi ya Kimkakati katika Jiji la Dodoma na ile ya muda mfupi na ya kati ili kuhakikisha wananchi wa Dodoma kwenye maeneo yenye changamoto ya Majisafi wanapata huduma ya maji.
Post A Comment: