Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Dkt Salehe Mkwizu (PhD) ametatua kero ya abiria dhidi ya wajasiriamali wachoma mahindi ambao wamekuwa na mtindo wa kutumia mabanda ya kupumzika abiria kama sehemu yao ya kuchomea mahindi.
Mhe. Dkt Mkwizu amewaelekeza maeneo ambayo wanaweza kutumia kwa ajili ya kazi hiyo wakati mchakato wa kuandaa eneo maalum kwa ajili yao unafanyika.
Dkt. Mkwizu akiwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Fedha wamewataka kuhama mara moja katika mabanda hayo kwani imekuwa kero ambapo abiria wanapata vumbi ya majivu wakati wa upepo
Pia Mheshimiwa Mkwizu amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuandaa mazingira rafiki kwa kutengeneza eneo ambalo wafanyabiashara hao watakaa na kufanya biashara zao vizuri kwa kutengenezewa mabanda yenye kuwa na bati ili waweze kufanya kazi wakati wote wa mvua na jua.
Post A Comment: