Mkuu wa Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Bi.Dina Mathamani amewataka maafisa utumishi wa wilaya hiyo kuwajibika katika kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi kwa kuibua changamoto wanazokutana nazo katika maeneo yao.

Hayo yamejiri katika mafunzo ya Elimu ya uraia na utawala bora yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Akizungumza katika mafunzo hayo Bi.Mathamani amesema kuwa ili watumishi hao waweze kufanya shughuli zao vizuri ni lazima suala la utawala bora liweze kuzingatiwa ili wananchi wajue vitu wanavyovihitaji katika nchi yao.

Kwa upande wake Bw.Hamis Mjanja kutoka ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa, amesema kuwa lengo la kufanya mafunzo hayo ni kukumbusha wajibu wa kila kiongozi katika utekelezaji wa majukumu aliyopewa na serikali .

Bw.Mjanja Amesema kuwa ni muhimu kwa viongozi wa serikali kufanya kazi kwa kuzingatia suala la utawala bora

Nao baadhi ya washiriki waliohudhuria akiwemo Hedetrides na Frank Michael ambao ni watendaji wa kata, wamesema mafunzo waliyopata leo watayafanyia kazi kwa kuzingatia misingi na weledi hususani katika suala la utawala bora na sheria.

Mafunzo hayo yanayoratibiwa na wizara ya katiba na sheria katika mikoa mitano na kwasasa yanaendelea kufanyika katika mikoa sita na hivyo kukamilika kwake kutaongeza idadi na kufanya mikoa kumi na moja kuwa imefikiwa na mafunzo haya.

Mikoa ambayo mafunzo hayo yanafanyika kwa sasa ni pamoja na mikoa ya Kigoma, Kilimanjaro, Geita, Katavi, Tabora na Mtwara




Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: