MBUNGE wa Jimbo la Korogwe vijijini Timotheo Mnzava amechangia kiasi cha Shilingi lakini tano (500,000) kwaajili ya kuweka Malumalu katika kanisa la la Kiinjili la Kilutheli Tanzania 'KKKT' Makumba lililopo wilayani Korogwe ambalo bado ujenzi wake unaendelea ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa hivi karibuni.
Mzava ambaye alishiriki Ibada katika kanisa hilo January 5,2025 kabla ya kuanza ziara yake na kuzungumza na wananchi kwenye mikutano ya hadhara katika maeneo ya Makumba , Mayuyu na Magoma amewapongeza waumini ambao walianza ujenzi huo tangu awali mpaka hatua hiyo lilipofikia likiwa limeshaanza kutumika.
"Ujenzi wa kanisa hili mpaka kufika hapa maana yake kuna watu wametumia nguvu zao walijitoa kwa hali na mali kwa kazi hii naamini Mungu anendelea kuwabariki na niwapongeze sana kwa kazi kubwa ya Mungu ambayo waliiifanya"
"Nitawaunga mkono kwenye kazi hii ya ujenzi, nimeambiwa unaoendelea kazi inayofanyika sasa ni kuweka Malumalu na mimi nitachangia sehemu ya kazi hiyo ili niwe sehemu ya uboreshaji wa miundombinu ya kanisa hili kama sadaka yangu" alisema Mzava
Aidha pamoja na kazi zinazofanywa na kamati za ulinzi na usalama katika kuwahakikishia watanzania amani amewataka waumini wa kanisa hilo kuendelea kuliombea nchi amani hususani mwaka huu kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Madiwani , wabunge na Rais.
"Sote kwa ujumla tuendelee kusimama kwenye nafasi zetu kuiombea sana nchi yetu ili iendelee kuwa mahali salama sisi kama watanzania Mwenyezi Mungu ametupa neema katika nchi ambazo zipo kwenye mazingira mazuri ya utulivu na amani, na utulivu huu si kwa sababu tu ya vyombo vya usalama bali wapo watu wa Mungu ambao wanatumia nafasi zao ili kuliombea amani nchi yetu tuendelee kuliombea amani Taifa letu" alisema
Mchungaji wa kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania 'KKKT' Makumba, Richard Mkufya amemshukuru Mbunge kwa mchango huo ambao utakwenda kumaliza sehemu ya uwekaji wa Tairizi ambao tayari wameshaanza kuweka kwa mchango iliyokuwa ikitolewa na waumini wa kanisa hilo .
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye shule ya msingi Makumba Diwani wa kata ya hiyo Idd Shebila amesema pamoja na jitihada zilizofanywa na Serikali katika kuwasogezea karibu huduma wananchi bado kuna changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Zahanati ya Kijiji hicho
"Hii zahanati ya kijiji ambayo ndiyo kongwe katika wilaya yetu ya Korogwe lakini mvua inaonyesha bati linavuja tunahitaji ukarabati kubwa kwenye zahanati hii lakini pia Kuna uchakavu wa jengo la mama na mtoto tukuombe Mbunge wetu temnea na changamoto hii tupate ufumbuzi" alisema Shebila .
Akizungumza kwa niaba ya wananchi mwenyekiti wa kijiji Nikodemas Liondo amemuomba Mbunge kuwasaidia kupatiwa uelewa wa kutosha kuhusu gharama za mama wajawazito wanapofika katika kituo cha afya Magoma ambapo hutakiwa kulipia shilingi lakini mbili (200,000).
"Wakina mama wajawazito wanapofika katika kituo cha afya Magoma kwaajili ya kujifungua iliyokea kama wanatakiwa kujifungua kwa upasuaji anaambiwa ni lazima atoe shilingi lakini mbili tunaomba hili tupatiwe elimu ili tuweze kulifahamu zaidi"
Mmoja wa wananchi wa kata hiyo
"Bado zipo changamoto kwenye baadhi yawas maeneo lakini kama viongozi wetu ni jukumu letu kusimamia kuona changamoto hizo zinaisha ikiwemo changamoto ya ukosefu wa maji, miundombinu ya Zahanati na shule ya Sekondari Mzava yapo mengi ya kusema ikiwemo Umeme bado hayo yote tunaendelea nao na tunaamini yote yatafanyika kabla hatujamaliza mwaka huu"
"Serikali imetoka fedha kwaajili ya ununuzi wa vifaa Tina na magari ya kubebea wagombea katika hospitali yetu ya Magoma katika awamu hii tumepata gari tunaielekeza halmashauri gari hilo lielekezwa kwenye hospital ya Magoma"
Serikali ilikubali kutoa fedha kwaajili ya kujenga mabwawa na sisi watu wa Korogwe tutajenga mabwwaw mawili ikiwemo la Mayuyu ambalo lilihatobiiwa na mvua tumekubaliana ufanyike usanifu mpya wa haraka
Post A Comment: