Na Denis Chambi, Tanga.
MBUNGE wa Jimbo la Korogwe vijijini Timotheo Mnzava amechangia fedha kiasi cha shilingi Milion Moja (1,000,000) kwaajili ya ujenzi wa kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania 'KKKT' lililopo Makumba pamoja na Msikiti wa Alahamisi uliopo Magoma ikiwa ni mchango wake wa kuwaunga mkono wananchi katika nyumba hizo za ibada.
Akiwa katika kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania 'KKKT' Makumba ambapo alishiriki ibada iliyofanyika jumapili January 5, 2025 kabla ya kuanza kwa ziara yake ya kutembelea na kuongeza na wananchi jimboni Mnzava amewapongeza waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania 'KKKT' Makumba kwa majitolea yao ya hali na mali tangu kuanza kwa ujenzi wa kanisa hilo ambalo sasa limeshaanza kutumika.
"Ujenzi wa kanisa hili mpaka kufika hapa lilipo maana yake kuna watu ambao wametumia nguvu zao walijitoa kwa hali na mali kwaajili ya kazi hii naamini Mungu ataendelea kuwabariki na Mimi niwapongeze sana"
"Ujenzi wa kanisa hili nimeambiwa kazi inayofanyika sasa hivi ni kuweka Malumalu na mimi nitachangia shilingi lakini tano ikiwa ni sehemu ya kazi hiyo ya uboreshaji wa miundombinu kama sadaka yangu" alisema Mnzava.
Akizungumza kwa niaba ya waumini , mchungaji wa kanisa hilo Richard Mkufya amemshukuru Mbunge kwa mchango huo ambao utakwenda kuwaongezea nguvu katika kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo
Mbali na ujenzi wa nyumba hizo za ibada Mnzava pia amewapa kiasi cha shilingi lakini nne (400,000) kikundi cha wakina mama wanaofanya shughuli zao za ujasiriamali fedha ambazo aliwaahidi kuwashika mkono ili kuwawezesha kuongeza kipato chao.
Mbunge Mnzava amesisitiza kuwa jukumu la kulinda na kutunza amani si la vyombo vya ulinzi na usalama pekee bali kila mtanzania anapaswa kushiriki kuvilinda hususani mwaka huu wakati Taifa likielekea kwenye uchaguzi mkuu wa Madiwani wabunge na Rais.
"Sisi sote kwa ujumla tuendelee kusimama kwenye nafasi zetu kuiombea sana nchi yetu ili iendelee mahali salama sisi kama watanzania Mwenyezi Mungu ametupa neema katika nchi ambazo zipo kwenye mazingira mazuri ya utulivu, utulivu huu sio tu kwa sababu ya vyombo vya ulinzi na usalama bali wapo watu wa Mungu ambao wanatumia nafasi zao ili kuiombea amani nchi yetu
Post A Comment: