Kuelekea mkutano wa nishati wa wakuu wa nchi za Afrika, Tanzania imeweka historia kwa kuwaunganishia umeme wananchi kwa asilimia 78.4 ambapo kwa vijijini uunganishaji umefikia asilimia 100 na kwenye vitongoji umefikia asilimia 52.3 huku ikitarajiwa kuwa Watanzania milioni 13.5 watasambaziwa umeme ifikapo 2030.

Mha. Olotu amesema kuwa  idadi ya watu nchini baada ya kufanyika Sensa  ya Watu na Makazi iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kuwa Tanzania inakadiriwa kuwa na watu milioni 60 na kwa taarifa ya umeme asilimia 78.4 ya watanzania wameunganishwa na umeme. 

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (REA), Mha. Jones Olotu jijini Dar es Salaam. 

Amesema kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umesema kuwa vijiji vyote 12,318 ambayo ni sawa na asilimia 100 vimefikiwa na umeme.

Aidha, Tanzania Bara ina jumla ya vitongoji 64,359 ambapo tayari vitongoji 33,657 sawa na asilimia 52.3 vimefikiwa na umeme na vitongoji 30,702 vilivyobaki vipo kwenye mpango wa kupatiwa umeme. 

Ameongeza baadhi ya faida za mkutano huo kuwa ni pamoja na kuongezeka idadi ya  Watanzania watakaounganishwa na umeme ifikapo mwaka 2030 hadi kufikia milioni 13.5 kutoka milioni 5.2 ya sasa.

Ameongeza kuwa, Wakuu wa Nchi 54 kutoka Bara la Afrika na viongozi wengine watashiriki mkutano huo wakiwemo Mawaziri wa Fedha na Nishati kutoka barani Afrika.

Ameongeza kuwa, mkutano huo unafanyika nchini kwa sababu Rais Samia ni kinara wa nishati safi ya kupikia duniani na katika sekta nzima ya nishati Rais Samia amefanya mengi kwa watanzania. 

Mkutano huo utaenda sambamba na Maonesho yatakayofanyika tarehe 27 na 28 Janauari, 2025 katila ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.

Share To:

Post A Comment: