Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} katika kata za Mirerani na Endiamtu Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wamesikitishwa na hatua ya Katibu wa Chama hicho ngazi ya Wilaya,Amos Shimba kuingilia kati uchaguzi na kukiuka taratibu za uchaguzi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mirerani na wameomba viongozi wa juu wa chama kumwondoa katibu huyo kwa kuwa yuko kwa ajili ya maslahi yake na sio ya chama.
Uchaguzi wa Mwenyekiti,Makamu na wajumbe wa Mji huo unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu na taratibu zote za kichama zilifanyika ikiwa ni pamoja na wanachama kuchukua fomu na kurudisha lakini baadhi ya majini kukatwa bila ya kutolewa sababu kwa maelekezo ya katibu huyo.
Akizungumza na gazeti hili katika Mji wa Mirerani,Hussein Bakari alisema kuwa waliochukua fomu na kurudisha kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji wa Mdogo wa Mirerani walikuwa wanachama wa CCM watabi ambao ni pamoja na Christopher Chengula kutoka kata ya Mirerani,Hamad Mallya kutoka kata ya Endiamtu.
Kwa mujibu wa Bakari wengine waliochukua fomu na kurudisha kuwania kiti hicho ni pamoja na Omari Hussein kutoka kata ya Endiamtu,Adamu Kobelo kutoka kata ya Endiamtu na Hans Nkya kutoka kata ya Endiamtu.
Alisema cha kushangaza waliorudishwa kuwani nafasi hiyo wote ni kutoka kata ya Endiamtu ambao ni pamoja na Omaru Hussein,Hans Nkya na Hamad Malya na kusema kuwa baadhi ya viongozi wa CCM ngazi ya kata kulazimishwa kuingiza majina ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wakati sio wanachama wa chama hicho na njama hizo zinadaiwa kufanywa na Katibu Shimba.
Bakari alisema katika nafasi ya uteuzi ya mwicho kichama aliteuliwa Hans Nkya kuwania nafasi ya Mwenyekiti na Makamu alichaguliwa Primu Shirima na uchaguzi kufanyika bila idadi ya wajumbe kukamilika kwani mkutano huo unapaswa kuhudhuriwa na wajumbe 35 wakiwemo madiwani lakini uchaguzi wa kuwapitisha wagonbe hao walihudhuria wajumbe 15 kinyume na kanuni za chama.
‘’Tunajua njama zote za Katibu Shimba juu ya uchaguzi huo na tunajua mbinu za hovyo anazofanywa kwa maslahi yake na hiyo inajenga chuki kwa wanachama wa CCM Mirerani kukikataa chama hivyo tunaomba viongozi wa juu waliingilie kati ikiwa ni pamoja na kumwondoa kwa kuwa yuko kimaslahi’’ alisema Bakari
Naye Mwanachama Alphonce Mollel mkazi wa kata ya Endiamtu alisema Katibu Shimba anambeba mmoja wa wagombe anayefanya kazi kwenye kampuni kubwa ya madini{jina tunalo} na ameaidiwa fedha nyingi akichaguliwa na ndio maana anaingiza wapiga kura feki kwa kuwalazimisha makatibu kata wa CCM kuingiza katika leja wapiga kura feki ili kutimiza matakwa yake.
Mollel alisema mbali ya kufanya hivyo kata za Mirerani na Endiamtu pia Katibu Shimba amefanya hivyo katika Kata ya Shambarai kwa kuingiza viongozi ambao hawakuchaguliwa na wana CCM na kuingiza wa kwake ili kulinda kaampuni hiyo ya madini ifanye kazi bila bugudha.
Akizungumzia tuhuma hizo kwa njia ya simu ya kiganjani,Katibu Shimba alisema sio za kweli kwani zina lengo la kumchafuaa kwani taratibu zote za mchakato wa uchaguzi kuanzia uchukuaji,urudishaji na uteuzi zilifuata taratibu na kama kuna mgombea anaona hajatendewa haki kuna taratibu za kufanya ndani ya chama na sio kukimbilia kwenye vyombo vya habari.
Shimba alisema wajumbe 17 wa uchaguzi walihudhuria mkutano wa uchaguzi na idadi hiyo ilikuwa nusu la kolamu ya wajumbe wa Mkutano Mkuu hivyo kanuni za chama zinathibitisha kufanyika Mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Simanjiro,Kiria Laizer alipoulizwa juu ya tuhuma za katibu wake kufanya njama za kuingiza majina feki ya wapiga kura na kusimamia kwa asilimia mia moja uchaguzi haramu alisema sio za kweli kwani katibu wake alisimamia taratibu na kanu za uchaguzi na kusema wanamtuhumu hawana hoja za msingi wanapaswa kijipanga katika cchaguzi zijazo.
Laizer alisema kama kuna wanachama wanalalamikia uchaguzi na kumtuhumu Katibu kuna taratibu za kufuata ndani ya chama na kutoa nje malalamiko ni ukiukwaji wa taratibu na wakigundulika hatua kali zitachukuliwa katika vikao vya maadili.
Alisema Katibu ametimiza wajibu wa kikanuni na kinachofuata kwa sasa ni uchaguzi wa serikali kufanyika ikiwa ni pamoja na jina la Nkya kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Simanjiro ili uchaguzi ufanyike.
Post A Comment: