Na Joseph Mahumi, WF, Dar es Salaam.


Rais wa Benki ya Dunia (WBG), Bw. Ajay Banga amewasili nchini mchana wa leo tarehe 26 Januari 2025, Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ujulikanao kama “Mission 300”, utakaofanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
 
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Bw.Banga amepokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Cosato Chumi kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe.Dkt. Elsie Kanza, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bw. Nathan Belete, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali. 
 
Mkutano huo unatarajiwa kuwa utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi 25 na Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu na Naibu Mawaziri Wakuu 10 inafanya idadi ya viongozi wa ngazi ya juu kufikia 35 na utajadili namna ya upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa watu milioni 300 barani Afrika ifikapo mwaka 2030.
Share To:

Post A Comment: