Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imefurahishwa na usimamizi mzuri wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Halmashauri hiyo ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari ya Bumva iliyopo kata ya Segese.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mh. Ibrahim Six mbele ya wajumbe wa kamati hiyo aliyoambatana  nayo wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayo endelea ndani ya Halmshauri ya Wilaya ya Msalala.

Mradi huo wa ujenzi wa shule ya Sekondari Bunva  umeghalimu jumla ya Tsh.  603,890,563 ambazo zimeletwa kutoka Serikali kuu. Mradi huu unatekeleza ujenzi wa Vyumba nane vya madarasa, jingo la utawala lenye ofisi mbili za walimu, jengo la TEHAMA, majengo mawili ya maabara yenye maabara ya fizikia, kemia na biolojia, tanki la maji la ardhini, vyoo na kichomea taka. Mradi huo upo hatua za umaliziaji ambapo unatarajia kuanza kutumika ifikapo mwezi Aprili 2025.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Bi. Rose ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Samia Suluhu Hassan,  ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha za kufanikisha ujenzi huo ambazo zitasaidia kupunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu katika shule ya Sekondari ya Mwalimu Nyerere na Shule ya Sekondari ya Segese.









Share To:

Post A Comment: