Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea na jitihada zake katika kukuza ushirikiano wa Kidemokrasia na Mataifa ya nje, na hivyo kuinua Sekta ya Utalii na Uwekezaji nchini.

Katika kutekeleza azma hiyo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi amefanya mazungumzo na Balozi wa Japan na kusema kuwa, Tanzania na Japan zitaendelea kushirikiana kwa kuanza kufundisha Lugha ya Kiswahili nchini Japan.

Prof. Kabudi ameyasema hayo wakati alipokutana na Balozi wa Japani  hapa nchini Yasush Misawa, anayemaliza muda wake, wakati alipotembelea Wizara hiyo.

#KAZIINAONGEA

Share To:

Post A Comment: