Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Cde. Jokate Mwegelo amechangia Shilingi milioni tatu katika mfuko wa vijana maofisa usafirishaji maarufu Bodaboda katika kituo cha Sabasaba A mkoani Dodoma.
Bodaboda hao wanaofahamika pia kwa jina la kituo chao VIJANA NA SAMIA leo walipata ugeni huo rasmi ambao walizindua shina la Wakereketwa la UVCCM la Vijana wa Samia soko la Sabasaba na kibanda kwa ajili ya kupumzikia wakati wa jua na mvua ambacho kimejengwa na Mbunge wa Dodoma, Ndg. Anthony Mavunde.
Cde. Jokate kabla ya kufika katika uzinduzi huo aliongozana na vijana zaidi ya 500 ambao wamekuwa wakisaidia maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa utakaofanyika tarehe 18 hadi 19 Januari, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.
Cde. Jokate amewataka vijana hao kuendelea kuamini serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani imekuwa ikithamini vijana katika kila sekta kuhakikisha wanapiga hatua katika shughuli za uzalishaji.
Post A Comment: