Mwanachama wa Yanga na
mdau wa soko, Hussein Makubi Mwananyanzala, ameonyesha furaha yake kwa wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa CCM kwa hatua yao ya kumchagua na kumpendekeza Rais Samia
Suluhu Hassan kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka
huu.
Akizungumza na
waandishi wa habari mkoani Geita, Mwananyanzala amepongeza mafanikio makubwa
yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia katika kipindi kifupi cha uongozi
wake. Ameeleza kuwa Rais Samia amefanikisha mageuzi makubwa ya kimaendeleo
katika sekta mbalimbali, ikiwemo: Sekta ya Madini – Kuruhusu utoaji wa leseni
nyingi kwa wachimbaji wadogo, jambo lililoongeza fursa na ajira kwa Watanzania
wengi.Uboreshaji wa Miundombinu – Ujenzi wa madaraja makubwa na kuboresha
miundombinu ya umeme kote nchini.
Hussein Mwananyanzala
ameendelea kwa kuwaomba wananchi kumchagua Rais Samia Suluhu Hassan kwa kura
nyingi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, akisema kuwa anaamini Rais Samia
ataendeleza juhudi za kuwaletea maendeleo Watanzania wote.
"Mafanikio
tuliyoyashuhudia yanahitaji kuendelezwa, na Rais Samia ni kiongozi ambaye
ameonyesha dhamira ya dhati ya kutufikisha mbele zaidi," aliongeza.
Post A Comment: