NA EMMANUEL MBATILO, KOROGWE TANGA

TAASISI ya HakiElimu imezindua Mradi wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia katika elimu ambao umelenga kuboresha Miundombinu ya Maji, Usafi wa Mazingira pamoja na Kupunguza Ukatili wa Kingono na Kijinsia ili Kuhakikisha Wasichana Wanaendelea na Masomo na kutimiza ndoto zao za kielimu.

Mradi huo unaofadhiliwa na serikali ya Canada kupitia idara ya uhusiano wa kimataifa ‘global affairs Canada’ unategemea kugharimu takribani dola za Canada milioni 4.5 sawa na takribani shilingi billioni 7.8 za Kitanzania.

Akizungumza Januari 23, 2025 Wilayani Korogwe, wakati akizindua Mradi huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mkuu wa Wilaya Korogwe, William Mwakilema amesema wataendelea kutoa ushirikano kupitia mradi huo ili kufanikisha utekelezaji na upatikanaji wa matokeo yaliyokusudiwa.

Amesema ni muhimu kwa wananchi na Halmashauri kuuelewa mradi na kuendelea kufuatilia na kutoa ushirikano katika maeneo mnayopaswa.

"Kwa wale mtakaopata mafunzo ni wajibu wetu kuitumia elimu hiyo kuleta mabadiliko tarajiwa ikiwa ni pamoja na kuwaambukiza wengine ambao hawatabahatika kuwa sehemu ya utekelezaji wa mradi huu. Nitafurahi kusikia, mafunzo na mbinu zilizopatikana, mnazipeleka pia katika shule ambazo hazipo kwenye mradi ili kutanua wigo wa mradi". Amesema

Aidha ametoa maagizo kwa watendaji ngazi ya Halmashauri na Shule, katika maeneo ambayo mradi utajenga miundombinu na kutoa vifaa vya kujifunza na kufundishia, kuvitunza kwa wivu mkubwa ili kuweza kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

Pamoja na hayo amewapongeza HakiElimu kwa kupata ufadhili wa mradi huu wa zaidi ya dola za Canada Milioni Nne na Nusu (4,500,000) kwa miaka hii mitano kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kitanzania.

Ameishukuru Serikali ya Canada kupitia kwa Balozi na mwakilishi wa Balozi wa Canada Nchini Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Mahusiano ya Kimataifa (Head of Cooperation) wa Serikali ya Canada kwa kufadhili mradi huo muhimu wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia katika Elimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu, Dkt. John Kalage amesema mradi huo utatekelezwa katika shule za msingi 16 na shule za sekondari 24 katika wilaya nane kwenye mikoa nane kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara ambazo ni pamoja na Wilaya ya Korogwe-Tanga, Mkuranga-Pwani, Kilosa-Morogoro, Mpwapwa-Dodoma, Babati-Manyara, Iramba-Singida, Muleba-Kagera na MusomaMara.

"Mradi unatarajiwa kuwafikia wasichana 12,240 na wavulana 11,760 (wenye umri kati ya miaka 10 hadi 19) ambao ni walengwa wakuu wa mradi. Mradi, pia utawahusisha walimu 100 kutoka shule hizo 40, na wajumbe 16 wa vikundi vya Marafiki wa Elimu wanaosimamia utekelezaji wa shughuli za kila siku shuleni na katika jamii". Amesema Dkt. Kalage

Amesema mradi huo utawafikia takribani wanajamii 140,000 na maafisa 320 wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGA) kupitia mijadala ya kijamii na mafunzo ya kujengea uwezo, yenye lengo la kuongeza uelewa kuhusu kuzuia ukatili wa kijinsia (GBV) na umuhimu wa kukuza usawa wa kijinsia katika elimu.

Hata hivyo amesema kuwa pamoja na juhudi kubwa za Serikali katika kuboresha elimu, bado shule nyingi zinahitaji maboresho makubwa katika mfumo wa maji, miundombinu na vifaa vya usafi wa mazingira.

Ameeleza kuwa Mradi huo utatekelezwa kwa kushirikiana na Serikali na jamii husika.

Pamoja na hayo amesema HakiElimu itachangia katika kuweka vifaa vinavyozingatia mahitaji ya kijinsia katika shule 40 za mradi, kwa manufaa ya wanafunzi wanaokadiriwa kufikia 24,000 (wavulana na wasichana). HakiElimu itawekeza katika ujenzi wa visima vya maji na kujenga vyoo vya wasichana vilivyo na vyumba maalum vya kubadilishia nguo.

Nae Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Canada, Carol Mundle amesema wanajivunia kuwa sehemu ya mafanikio ya uwanzishwaji wa mradi huo.

Amesema maendeleo ambayo yametokea katika uanzishwaji wa miradi hiyo ni pamoja na kuongeza kwa ufahuru wa wanafunzi,

Hata hivyo ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kufikia usawa wa kijinsia kwenye maeneo ya uandikishwaji mashuleni hivyo amewahimiza wazazi na walimu kushirikiana na HakiElimu kwani wao ndo waendeshaji wa mradi huo.

Malengo mahususi ya Mradi huo ni kujenga mazingira salama na yanayozingatia mahitaji ya kijinsia katika shule za mradi, Kuimarisha ulinzi dhidi ya unyanyasaji wa kingono na kijinsia hasa kwa wasichana katika shule pamoja na Kuimarisha miundombinu, upatikanaji wa vifaa safi na salama vya usafi wa mazingira vinavozingatia mahitaji ya kijinsia.
Mkuu wa Wilaya Korogwe, William Mwakilema (kushoto) akiwa na Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Canada, Carol Mundle (kulia) wakivuta kitambaa kuzindua Mradi wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia katika elimu Januari 23, 2025 katika shule ya Sekondari Buna iliyopo Korogwe mkoani Tanga. Mkuu wa Wilaya alizindua kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Mkuu wa Wilaya Korogwe, William Mwakilema (kushoto) akiwa na Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Canada, Carol Mundle (kulia) wakivuta kitambaa kuzindua jiwe la msingi la ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Buna  Januari 23, 2025 katika shule hiyo iliyopo Korogwe mkoani Tanga. Mkuu wa Wilaya alizindua kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga

Mkuu wa Wilaya Korogwe, William Mwakilema (kushoto) akiwa na Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Canada, Carol Mundle (kulia) wakipongezana mara baada ya kuzindua jiwe la msingi la ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Buna  Januari 23, 2025 katika shule hiyo iliyopo Korogwe mkoani Tanga. Mkuu wa Wilaya alizindua kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Pembeni ni Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu, Dkt. John Kalage. 
Mkuu wa Wilaya Korogwe, William Mwakilema akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia katika elimu Januari 23, 2025 katika shule ya Sekondari Buna iliyopo Korogwe mkoani Tanga. Mkuu wa Wilaya alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Canada, Carol Mundle akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia katika elimu Januari 23, 2025 katika shule ya Sekondari Buna iliyopo Korogwe mkoani Tanga. 
Mwenyekiti wa Bodi - HakiElimu CPA. Sylvester Orao akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia katika elimu Januari 23, 2025 katika shule ya Sekondari Buna iliyopo Korogwe mkoani Tanga. 
Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu, Dkt. John Kalage akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia katika elimu Januari 23, 2025 katika shule ya Sekondari Buna iliyopo Korogwe mkoani Tanga. 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Yusuph Kallaghe akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia katika elimu Januari 23, 2025 katika shule ya Sekondari Buna iliyopo Korogwe mkoani Tanga. 

Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu, Dkt. John Kalage akiwa na Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Canada, Carol Mundle wakicheza ngoma pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Buna wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia katika elimu iliyofanyika Januari 23, 2025 katika shule hiyo iliyopo Korogwe mkoani Tanga. 

Mkuu wa Wilaya Korogwe, William Mwakilema pamoja na wadau wengine wa elimu wakipata picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya HakiElimu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia katika elimu iliyofanyika Januari 23, 2025 katika shule ya Sekondari Buna iliyopo Korogwe mkoani Tanga. 
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Buna wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia katika elimu iliyofanyika Januari 23, 2025 katika shule hiyo iliyopo Korogwe mkoani Tanga. 

Baadhi ya matukio katika picha kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Mageuzi ya Usawa wa Kijinsia katika elimu iliyofanyika Januari 23, 2025 katika shule ya Sekondari Buna iliyopo Korogwe mkoani Tanga. 

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: