Na Denis Chambi, Tanga.

MBUNGE wa Jimbo la Korogwe vijijini Mkoani Tanga Timotheo Mnzava amemuelekeza mganga Mkuu wa wilaya hiyo kuchukua hatua dhidi ya watumishi wa kituo cha afya Magoma wanaodaiwa  kuwalipisha wamama wajawazito kiasi cha shilingi lakini mbili (200,000) pale wanapohitajika kufanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua jambo ambalo ni kinyume na maelekezo ya Serikali.

Agizo hilo linakuja kufuatia malalamiko ya wananchi wa kata ya Magoma wilayani Korogwe wakati wa ziara ya Mbunge huyo ambayo aliifanya  January 5,2025 katika kituo hicho kwa lengo la  kukabidhi gari ya wagonjwa  'Ambulance' iliyotolewa na Serikali  ambapo watumishi hao wanaodaiwa kuwatoza wagonjwa kiasi hicho, wengine na wengine huchangia shilingi elfu 10,000 pale wanapoanza Kliniki.

"Mganga Mkuu wa wilaya tenga siku kaa na watumishi wa kituo cha afya Magoma tunahitaji tuwaone wanabadilika na wanatimiza wajibu wao, viongozi wa kisiasa wanatukanwa kwa sababu ya uzembe wa watumishi tumesikia kuna watu wanalipa mpaka lakini mbili kufanyiwa upasuaji  maelekezo ya Serikali wanaostahili kuhudumiwa bure wahudumiwe bure wanaostahili kulipa walipe kama maelekezo ya Serikali yanavyotaka" alisema Mnzava.

Akizungumzia Gari hiyo ya wagonjwa Mnzava ameelekeza isitolewe nje ya kituo cha afya Magoma pasipo utaratibu maalum  huku akipiga marufuku wananchi kulipishwa fedha za mafuta pale wanapohitaji huduma ya dharura kupelekwa kituo kingine kwaajili ya matibabu zaidi.

"Kwa kuwa gari hili limetolewa na Serikali kwaajili ya wananchi wa Magoma , isije ikatokea gari hili likaenda kufanya kazi wilayani , kituo chake cha kazi ni hapa kituo cha afya Magoma,  ni ruksa kuazima gari hii ikahudumie watu wengine lakini ni lazima itoke kwa utaratibu na irudishwe kwa utaratibu unaofaa"

"Hatutaki tusikie kwamba kuna mwananchi amelipishwa  fedha ya mafuta ya gari ya wagonjwa fedha ya mafuta inatolewa na halmashauri na sio mgonjwa , ikitokea gari imekosa mafuta nipigieni simu nitatoa mafuta mimi mwenyewe" amesisitiza Mnzava.

Wakieleza namna wanavyotozwa fedha hizo wakati wakiwa katika kituo cha afya Magoma baadhi ya wananchi akiwemo Omari Kipipa pamoja na Amina  Ramadhani  wamesema jambo hilo ni la muda mrefu wakiomba Serikali kuingilia kati huku wakiishukuru kwa kupatiwa Gari ya wagonjwa ambayo wamekuwa wakiiomba kwa muda mrefu baada ya gari waliokuwa wakilitumia awali kuharibika.

"Kituo cha afya Magoma kuna ubadhilifu mkubwa unaofanyika kila tukienda  kuhitaji huduma unapolipa haupati risiti unaambiwa mashine inaa matatizo sisi kama wananchi tumeona pale kuna udanganyifu, tunalipishwa mpaka shilingi lakini mbili tunapopeleka wagonjwa hususani wajawazito tunaomba  haya yafwatiliwe kwa kina" alisema Kipipa.

"Tunaishukuru sana Serikali Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge watu kutupambani kupata gari ya kubebea wagonjwa tumefurahi mno"

Kaimu mganga Mkuu wa  Halmashauri ya wilaya ya Korogwe Majaliwa  Tumaini ameeleza kuhusu matibabu yanayotolewa bure ngazi za vituo vya afya  na zahanati hususani kwa mama na mtoto pamoja na wajawazito kauli ambayo imekuja kuthibitishwa upigaji wa watumishi wanaowatoza fedha wananchi kwaajili ya matibabu.

"Kulingana na muongozo wa Serikali uliyotolewa mwaka 2022  upasuaji mdogo kwa ngazi ya Kituo cha afya  ni shilingi 20,000  upasuaji mkubwa ni shilingi 85,000 kwa zile dawa na vifaa ambavyo vinapatkana pale kituoni  lakini kama hazipo itakulazimu ununue nje ya eneo ambapo itamghalumu anayehudumiwa" 

" Watoto chini ya miaka mitano  na mama mjamzito huduma zao zinafolewa bure kwenye changamoto ambayo inahusiana na uzazi upasuaji unaohusiana na uzazi ni bure kabisa   kama kuna gharama nyingine nje ya hizo hayo ni makosa, lakini kama kuna vituo vipo nje ya kituo mgonjwa atalazimika akanunue" alisema Tumaini. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa  UWT  wilaya ya Korogwe  Hadija Mshahara ameahidi kufanya ziara za mara kwa mara katika kituo hicho pamoja na hosipitali ya wilaya ya Korogwe kufwatilia jambo hilo ambalo limekuwa ni kilio cha wananchi.

"Zipo siasa hapo kituo cha afya Magoma zinahatibiwa na watu wachache zinaihatibu na Serikali yetu  wakina mama wajawazito wanayozwa fedha  wakati huduma zao ni bure kituo cha afya ni pachafu mmno Serikali inayoa ruzuku kwenye dawa na vifaa tiba  nitafuatilia kama mwenyekiti wa UWT na gari hili la wagonjwa lisije likawa ni gari ya watu binafsi " alisema Mshahara 
Share To:

Post A Comment: