Na. Saidina Msangi, WF, Ngorongoro, Arusha.
Wizara ya Fedha inaendelea na Program ya kutoa elimu kwa Umma ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo Sekta ya Fedha 2020/21 - 2029/30 ambapo unalenga kufikia wananchi asimia 80 hadi kufikia mwaka 2025/26 pamoja na utekelezaji wa Programu ya Elimu ya Fedha kwa Umma ya mwaka 2020/21 - 2025/26.Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, imeifikia jamii ya Wamaasai katika Kijiji cha Nainokanoka na Endulen katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha na kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini.
Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akifafanua kuhusu njia sahihi za kutunza fedha, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Kijiji cha Nainokanoka, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Bi. Gloria Nampesya, akifafanua jinsi ya iusajili vikundi vya wajasiriamali, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Kijiji cha Nainokanoka, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga, na Mwenyekiti wa Kijiji cha Endulen Bw. Thomas Kadogoo, wakimkabidhi zawadi ya fulana, Bi. Norumoikoi Sanga, baada ya kujibu vizuri swali kuhusu akiba, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Kijiji cha Endulen, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Afisa Mauzo kutoka Benki ya NMB, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Bi. Njumali Lukumay, akiwaelekeza wananchi wa Endulen kufungua akaunti za kuweka akiba katika Benki ya NMB, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Kijiji cha Endulen, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Mkazi wa Kijiji cha Endulen Bi. Doric Toico, akieleza umuhimu wa kuweka akiba wakati akijibu swali lililoulizwa baada ya mafunzo ya elimu ya fedha, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Kijiji cha Endulen, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Endulen, wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwa njia ya filamu kuhusu elimu ya fedha, wakati Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Fedha iliyoambatana na Maafisa kutoka taasisi na wadau mbalimbali, ilipowasili kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha na kuhamasisha utumiaji wa huduma za fedha vijijini, katika Kijiji cha Endulen, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Post A Comment: