Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, akizunguza katika Ofisi ya Kaimu Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu na Mtakwimu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Jonas Mwita (hayupo pichani), baada ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kabla ya kuanza kutoa elimu ya fedha katika mkoa huo.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akizunguza katika Ofisi ya Kaimu Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu na Mtakwimu wa Mkoa wa Arusha Bw. Jonas Mwita (hayupo pichani), baada ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kabla ya kuanza kutoa elimu ya fedha katika mkoa huo.

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu na Mtakwimu wa Mkoa wa Arusha Bw. Jonas Mwita, akizunguza na Timu ya Wataalam wa kutoa elimu ya fedha (hawapo pichani), Ofisini kwake walipofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jijini Arusha, kabla ya kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wajasiriamali na wananchi wa mkoa huo.

Timu ya Wataalam wa kutoa Elimu ya Fedha, Kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Taasisi na wadau mbalimbali, ikiwa katika kikao maalum na Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu na Mtakwimu wa Mkoa wa Arusha Bw. Jonas Mwita, Ofisini kwake, walipofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wa mkoa huo.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro (wakwanza kulia) akimkabidhi Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu na Mtakwimu wa Mkoa wa Arusha Bw. Jonas Mwita, Nyenzo ya Kufundishia Elimu ya Fedha baada ya Timu hiyo ya kutoa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kufika katika Ofisi yake jijini Arusha.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, akitoa ufafanuzi kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wa Jiji la Arusha, kuhusu filamu ya elimu ya fedha yenye ujumbe kuhusu masuala ya uwekezaji, utunzaji wa fedha binafsi, kuweka akiba, kusajili vikundi vidogo vya fedha pamoja na masuala ya mikopo ambapo Timu ya wataalamu wa elimu wa fedha inatarajiwa kutoa elimu hiyo katika Mkoa huo.

Afisa Mwandamizi, Uchambuzi Fedha, Idara ya Sera, Utafiti na Mipango, kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA. Gladness Mollel, akitoa elimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wa Jiji la Arusha, kuhusu masuala ya uwekezaji.

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), mkoani Arusha, Bw. Josephat Komba, akieleza faida za wajasiriamali kujiunga na Mfuko huo, baada ya wajasiriamali hao kujitokeza katika Ukumbi wa Arusha Sekondari kwa ajili ya kupata elimu ya Fedha kutoka kwa Wataalam kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na taasisi na wadau mbalimbali.

Afisa Matekelezo uchangiaji hiari Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Arusha, Bi. Marietha Ngoma, akitoa elimu kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kuhusu uwekezaji kupitia mfuko huo, walipoungana na Timu ya Wataalam wa kutoa Elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Taasisi na wadau wengine jijini Arusha.

Baadhi ya wajasiriamali na wananchi wa jiji la Arusha wakipata elimu ya fedha kwa njia ya filamu yenye maudhui kuhusu matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kupanga bajeti na kuitekeleza, umuhimu wa kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha , utunzaji wa fedha binafsi, umuhimu wa kushirikisha familia na watu wa karibu kwenye masuala ya fedha na uwekezaji, umuhimu wa kukata bima ya biashara na mali nyingine, filamu hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha lengo likiwa ni kusambaza elimu ya fedha kwa njia rahisi ya burudani ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa masuala ya huduma za fedha.
Share To:

Post A Comment: