Mradi wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kupikia, unaojengwa katika Kijiji cha Veyula, Dodoma, umepiga hatua kubwa tangu uliposajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) mwaka 2023. Kiwanda hicho, chenye uwekezaji wa takriban dola milioni 60 za Kimarekani, kinatarajiwa kuanza uzalishaji mwaka huu huku ujenzi na ufungaji wa vifaa ukiwa tayari umefikia asilimia 90.

Kukamilika kwa kiwanda hiki kutatoa ajira kwa watu wapatao 500, jambo linalotarajiwa kuchochea ukuaji wa kiuchumi na kuboresha maisha ya wakazi wa Dodoma na maeneo jirani.

TIC imeendelea kuonyesha umuhimu wa huduma zake kwa kuhakikisha wawekezaji wanapata msaada wa haraka kusajili miradi yao na kuanza utekelezaji kwa wakati. Huduma hizi zimekuwa na mchango mkubwa katika kupunguza ucheleweshaji wa miradi na kuvutia uwekezaji zaidi nchini.

Hatua hii inaendelea kuifanya Dodoma kuwa kitovu cha uwekezaji nchini, ikithibitisha kuwa mazingira rafiki ya biashara yanaweza kuleta maendeleo ya haraka na endelevu.

 

Share To:

JOEL MADUKA

Post A Comment: