📌 Lengo ni kuhakikisha vinafanya kazi kwa ufanisi
📌 Ataka ukarabati wa mitambo Hale kumalizika kwa wakati
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu, amemtaka Mkandarasi anayekarabati mitambo katika kituo cha kufua umeme Hale kufanya kazi kulingana na makubaliano ya kimkataba ili kituo hicho kiweze kuingiza umeme wa kutosha kwenye gridi ya Taifa.
Dkt. Kazungu ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mitambo ya kufua umeme katika kituo cha Hale-Tanga, Nyumba ya Mungu- Moshi na New Pangani Falls ambapo ameisisitiza TANESCO kumsimamia ipasavyo mkandarasi.
"Lengo la ziara hii ni kukagua maendeleo ya Miradi hii ya umeme na kujionea hatua za ukarabati unaofanyika na nimemuagiza mkandarasi anayefanya ukarabati kufuata sheria na kanuni za mkataba ili kukamilisha kazi lakini pia ni lazima asimamiwe ili amalize kazi kwa wakati na kwa ufanisi." Amesema Kazungu
Meneja wa Vituo hivyo vya Kuzalisha umeme kwa njia ya maji, Mhandisi Kulwa Byemelo amesema "hali ya mitambo ya kuzalisha umeme ni nzuri katika kituo cha Nyumba ya Mungu ambacho kina uwezo kuzalisha jumla ya 8 MW.
Amesema kwa upande wa mitambo ya kuzalisha umeme ya kituo cha New Pangani Falls chenye uwezo wa kuzalisha 68MW mitambo hiyo ipo katika hali nzuri ya uzalishaji umeme.
Post A Comment: