Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund for Arab Economic Development), Bw. Albahar Waleed, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika, ulioanza leo tarehe 27 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo katika mazungumzo yao, walikubaliana kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali na Mfuko huo kupitia ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za maji, maendeleo ya miundombinu, na huduma jumuishi za kijamii. Kikao hicho kiliwashirikisha pia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba na Naibu wake, Bi. Amina Hamisi Shaaban, Mkuuwa Idara ya Mashariki ya Kati, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika, Mhe. Balozi Abdalah Kilima, Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait.
Share To:

Post A Comment: