MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amepokea taarifa maalumu ya mikakati ya uboreshaji wa Shule za Msingi Olympio Diamond, Zanaki Bunge, Mzizima na Kisutu ambayo imejikita kupunguza msongamano wawanafunzi kwa mwaka huu 2025 na kuinua taaluma.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Mpogolo amesema lengo ni kupunguza msongamano wawanafunzi, kuboresha kiwango cha utoaji elimu na mazingira bora ya kusomea na kufundishia ili kuendana na dhima ya uanzishwaji wa shule hizo na kukuza ufaulu.
Amesema, uboreshaji huo umejikita katika kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kujiunga na darasa la kwanza mwaka huu wa 2025.
Mpogolo, amesema taarifa hiyo inaonesha kwa upande wa Shule ya Msingi Bunge, wanafunzi walioandikishwa kujiunga darasa la kwanza mwaka huu ni wavulana ni 150 , wasichana 136 jumla kuu ikiwa ni 286.
Kwa upande wa Shule ya Msingi Zanaki, wavulana ni 153 wasichana 175 jumla kuu ikiwa ni 328.
Amesema Shule ya Msingi Kisutu, wavulana ni 138 wasichana 136 jumla ni 274 ambapo kwa upande wa Shule ya Msingi Mzizima wavulana 102 wasichana 108 jumla 210.
Amesema kwa shule zote hizo jumla ya wanafunzi walioandikishwa kwa mwaka huu 2025 ni 1,211.
Awali akikabidhi taarifa hiyo, Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Macha Manase, amesema kwa upande wa Shule ya Msingia Diamond, kwa mwaka huu wanafunzi walioandikishwa ni wavulana 131 tu na wasichana 125 jumla ikiwa ni 255.
Ameeleza mwaka jana idadi ya wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi katika shule hiyo ilikuwa ni wavulana 280 wasichana 242 jumla kuu 522 idadi ambayo ni kubwa.
Amesema katika Shule ya Msingo Olympio wavula 240, wasichana 260 jumla wanafunzi 500 ambapo waliomaliza elimu ya msingi mwaka 2024 walikuwa ni wavulana 395 wasichana 390 jumla kuu ilikuwa 785 idadi ambayo ilikuwa kubwa.
Post A Comment: