Mkuu Wa Wilaya Ya Mpanda Mkoa Wa Katavi, Jamila Yusuph Amesema Katika Wilaya ya Mpanda Zipo Changamoto Kadhaa katika utekelezaji wa Haki za Binadamu na Uzingatiwaji wa Msingi wa Utawala Bora Moja Ya Changamoto Hizo Ni Pamoja Na Uelewa Mdogo Wa Misingi Ya Haki Za Binadamu Miongoni Mwa Jamii Zetu ,Mila Na Destuli Kandamizi, Vitendo Vya Ukatili Wa Kijinsia, Vitendo Vya Ubakaji,Mauaji Na Imani Za Kishirikina.
Jamila Ameyabainisha hayo Wakati Akifungua Mafuzo Ya Kuwajengea Uwezo Viongozi Wa Serikali Za Mitaa Katika Manispaa Ya Mpanda Na Halmashauri Ya Wilaya Ya Nsimbo, Kuhusu Elimu Ya Uraia Na Utawala Bora.
Amesema Anaishukuru Wizara Ya Katiba Na Sheria Kwa Kuona Umuhimu Wa Kuendesha Mafuzo Kwa Walengwa, Ni Wazi Kuwa Mafunzo Haya Ni Muhimu Na Yatajenga Uelewa Kwa Viongozi Na Watendaji Kuhusu Masuala Uraia Na Utawala Bora.
“Rai Yangu Kwa Washiriki Ni Kuwa Mshiriki Kwa Ukamilifu Na Kutoa Maoni Na Mapendekezo Jinsi Ya Kuboresha Na Kukuza Masuala Ya Demokrasia Uzingatiaji Wa Haki Za Binadamu Na Utawala Bora”.
Kwa Upande Wake Wakili Wa Serikali Wizara Ya Katiba Na Sheria, Dorice Amesema Malengo Ya Kutoa Elimu Ya Uraia Na Utawala Bora Kwa Viongozi Wa Mamlaka Ya Serikali Za Mitaa Ni Pamoja Na Kuwajengea Uwezo Viongozi Wa Mamlaka Za Mitaa Za Usimamizi Wa Serikali, Wataalamu Katika Halmashauri, Viongozi Wa Serikali Za Mitaa Ili Kuongeza Na Kutekeleza Majukumu Kwa Kuzingatia Katiba Ya Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania.
Nae,Afisa Mipango Nuru Mwendapole kwa niaba ya Washiriki Anaipongeza Wizara Ya Katiba Na Sheria Kwa Kuleta Mafunzo Haya Kwa Maslahi Ya Wilaya Hiyo Na Mkoa Kiujumla, Kupitia Mafunzo Haya Yatawatoa Kutoka Hatua Waliyopo Kwaajili Ya Kuhudumia Vizuri Wananchi Ambao Wanawaongoza.
Post A Comment: