Na,Jusline Marco ; Arusha

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania NBAA, imeanza uboreshaji wa mitaala yake ili kuhakikisha inaendana na teknolojia ya kisasa na kufuata mifumo ya kidijitali na mabadiliko endelevu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo CPA Pius Maneno akizungumza katika mkutano wa pili wa Jumuiya ya Wahasibu wa Wakuu wa nchi za Afrika unaoendelea jijini Arusha pamoja na Maonesho, amesema katika Uboreshaji wa mitaala hiyo kutasaidia sekta ya uhasibu serikalini na katika taasisi binafsi kufanya kazi zao kwa usahihi.

Aidha amesema katika mkutano huo Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania NBAA, imeweza kuwasilisha mada mbalimbali zinazohusiana na taaluma ya uhasibu ikiwa ni pamoja na namna ambavyo NBAA imeisaidia Taaluma ya Uhasibu nchini katika kufikia malengo mbalimbali.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano na Mawasiliano kutoka NBAA Bi.Magreth Kageya amesema wakiwa kama washiriki wa mkutano huo wamejipanga kuhakikisha wanasogeza huduma karibu wadau wa uhasibu ili kuweza kutatua vhangamoto zinazoikabili taaluma hiyo.

Ester Isack Masala Idara ya Huduma kwa wanachama,Kitengo cha Usajili wa Wanachama NBAA ameeleza umuhimu wa madaraja ya uhasibu katika kukuza sekta hiyo.

Katika hatua nyingine Mhasibu Mwandamizi kutoka NBAA Simon Kyondo katika kuimarisha utrndaji kazi wa wahasibu na wakaguzi nchini Bodi hiyo imeweza kuanzisha kozi mpya mahususi kwaajili ya wakaguzi wa ndani.

Mkutano huo ambao umelifunguliwa na Waziri wa Ujenzi Mhe.Innocent Bashungwa, umeenda sambamba na kauli mbiu ya Kujenga Imani ya Umma katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Ukuaji Endelevu unatarajiwa kuhitimishwa hapo kesho.

Share To:

Post A Comment: