image.png

image.png
Na. Elimu ya Afya kwa Umma .

Wananchi kutoka maeneo mbalimbali katika Jimbo la Peramiho wameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Jenista Mhagama kwa kuanzisha  Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika Mkoa wa Ruvuma.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya Wananchi hao wamesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wana mchango mkubwa kwani kupitia Mpango huo elimu ya Afya  watakuwa wanapata kwa urahisi zaidi karibu na maeneo yao.
 
"Nashukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Mpango huu wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii eneo la Peramiho na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla pia nimshukuru Waziri wa Afya na Mbunge wangu wa Jimbo la Peramiho maana Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii huwa wanatusaidia sana  Elimu ya Afya kuhusu usafi wa mazingira na mambo mengine lukuki"amesema Deus Saule .

Afisa Mtendaji wa Kata ya Kilagano Norasco Mapunda amesema  Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika Kata ya Kilagano Jimbo la Peramiho Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wamekuwa na mchango mkubwa kwa jamii kutoa elimu ya Afya umuhimu wa kufunika turubai malori yanayobeba madini ya makaa ya mawe.

"Nashukuru Serikali kwa kutuletea Mpango huu Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ,kuna magari haya yanayobeba madini ya  makaa ya mawe,hawa CHW wametusaidia sana kutoa elimu umuhimu wa kufunika turubai ili kupunguza vumbi linaloweza kuleta athari kiafya mfano kukohoa, hivyo madereva wa magari hayo sasa wana uelewa wanafunika magari yao na elimu inatolewa kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano ya hadhara huu Mpango utaongeza msukumo katika elimu masuala mbalimbali ya Kinga katika Afya zetu"amesema.
Share To:

Post A Comment: