Na Denis Chambi, Tanga.

WANANCHI wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Wameiomba Serikali kuwapelekea huduma ya usafiri wa Boti  utakaowasaidia kufanya safari zao kwenda visiwani Zanzibar kwaajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo biashara.

Akizungumza mmoja wa wananchi wa Pangani Geoffrey Leonard mara baada ya waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa kufanya ziara katika eneo hilo amesema kuwa wakati mwingine hulazimika kutumia fiber boti na Majahazi kwaajili ya  kwenda Unguja licha ya kuwa Serikali ilishapiga marufuku usafiri huo ambao hutumia masaa zaidi ya 10.

"Tunaomba tupate walau  boti ambayo itatuwezesha wana Pangani kuweza kufika  Unguja  kwa haraka kwa sababu kwa sasa hivi watu wamekuwa wakitumia njia ambazo sio rasmi kwa sababu fiber boti zilizuiwa kusafirisha watu kwahiyo watu wengine ili kupata riziki wanachukua watu kwa njia ya magendo lakini tukipata boti itatusaidia wakati mwingine inatulazimu kupanda jahazi ambalo hutumia masaa mpaka 10 kwaajili ya  kufika Unguja" amesema Leonard 

Aidha Leonard amesema idadi kubwa ya wananchi wakiwemo vijana wanaofanya shughuli zao kwaajili ya kujipatia kipato  kando kando ya bahari wengi wakiwa  wanategemea kubeba mizigo  amesema kuwa  kwa sasa  hali imekuwa ni ngumu kwao kupata hata shilingi 5,000 kwa siku huku wakiwa wanategemewa na familiya jambo ambalo Wameiomba Serikali kuiangalia kwa upekee ili kuweza kuwasaidia.

"Kwa sasa eneo hili linakusanya zaidi ya watu 200 kwa siku, kazi zipo zinafanyika lakini kwa idadi ya watu ambao wapo na kazi zilizopo hazitoshelezi hata kwa kipato  kwa sababu ukiachilia  zao la Mkonge inayofuatia kuajiri watu nje ya daraja ni Bandari na wanapangani wengi sasa hivi wanategemea eneo la Bandari mizigo ambayo imekuwa ikija sio mingi ya kutosheleza kumewezesha mtu kupata kipato cha kutosheleza kwa matumizi ya familiya zao"

"Tumekuwa tukisikia kuwa Bandari zilizorasimishwa za Bagamoyo , Kunduchi na  Mbweni zinapokea mizigo mingi ombi letu na sisi tupate mizigo mingi kama wenzetu  walivyokiwa wanapata kwa lengo la kuweza kukimu familiya zetu"

"Vijana wengi sasa hivi shughuli za mtaani zimekuwa ni ngumu  kuweza kupata kipato macho yao yote yako hapa wakati mwingine inapota mpaka mwezi vijana kupata hata shilingi  elfu 5,000 kwao imekuwa ni ngumu na ukizingatia nyumbni umeacha  familiya  na inakutegemea    hii inatokana na kwamba kazi haziji kwa wingi" amesema Leonard.

Mbali na ombi hilo wameishukuru pia  Serikali kuwajengea Gati ambalo kwa sasa  limewezesha kusaidia kupakia mizigo kwa urahisi nayoelekea Unguja Visiwani Zanzibar ikiwemo Mkonge, Tanga stones pamoja na Mbao.

"Tuishukuru sana  Serikali kwa kutujengea Gati kwa sababu nje ya kupokea mizigo inayokuja kuna mizigo mingine inayopelekwa Unguja Gati limekuwa likirahisisha kupakia  mizigo katika vyombo vinavyosafirisha" alisema Leonard.

Kwa upande wake mmoja wa manahodha wanaoendesha usafiri wa Jahazi na Mashua  za mizigo kutoka Pangani kwenda Unguja Visiwani Zanzibar   wameiomba Serikali kuboresha  eneo lililojengwa Gati ambapo hulazimisha vyombo vya kupakia mbali kutokana na eneo lililopo kukaa mchanga  pamoja na uwepo wa Mwamba.

"Sehemu ambayo Boti zinatia nanga kwaajili ya kupakia mizigo huwa panajaa mchanga tunaomba Serikali pawe panachimbwa mara kwa mara  Kuna sehemu pia kuna mwamba lakini pia tunapongeza na kuishukuru Serikali kwa kutuona sisi wavuvi  tunatarajia kwamba ikitanuka baadaye tutapata faida zaidi"

Akizungumza Waziri wa  Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa mara baada ya kuwasikiliza wananchi hao amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali ili kuwasaidia wananchi kufanya shughuli zao katika mazingira rafiki ambapo mbali na  maboresho ya bandari hiyo  kukamilika kwa Barabara ya Kilomita 50 kutoka Tanga kwenda Pangani hadi Bagamoyo  kutatatua changamoto nyingi zilizokuwa zinawakabili.

"Tatizo kubwa  la Pangani kulikuwa ni Barabara  ambayo imekuwa ni changamoto ya kutoa mzigo hapa kwenda sehemu nyingine lakini baada ya Barabara hii kifunguka  tutaona mabadiliko makubwa na ndio sababu Serikali ikaamua kujenga Barabara hii na ndio kikwazo kikubwa  kukamilika kwake mtaona mabadiliko makubwa" amesema Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa kutokana na uhitaji mkubwa wa wananchi wa Pangani juu ya Boti  ya kwenda Unguja Zanzibar Wizara ya Uchukuzi  itakutana na Mamlaka ya Bandari Tanzania ' TPA'  pamoja na Wakala wa Meli Tanzania 'TASAC' kujafili na kuja na mpango wa pamoja ili kuwezesha usafiri huo.

""Bandari hii ilikiwa imelala kwa sababu kulikuwa hakuna Barabara   ndiyo inayoifungua bandari hii, kuhusu boti ya uokoaji hilo tumelisikia na tunaenda kulifanyia kazi tutakaa watu wa Bandari pamoja na na watu wa TASAC tutakuja na mapango maalum wa kuleta  boti"alisema Mbarawa.
Share To:

Post A Comment: