Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Lindi Patrick S. Magarinja akitoa elimu ya mahusiano bora baina chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali ili kukuza sekta ya elimu hapa nchini.
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Lindi Patrick S. Magarinja akitoa elimu ya mahusiano bora baina chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali ili kukuza sekta ya elimu hapa nchini
Baadhi ya walimu Makada wa CCM wakiwa kwenye mafunzo maalumu
Na Fredy Mgunda, Songwe.
Walimu makada wametakiwa kuwa mstari wa mbele Kwa kuhakikisha wanadumisha mahusiano mema baina yao na kati ya Chama na Serikali ili kukuza sekta ya elimu hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Lindi Patrick S. Magarinja wakati alipokuwa akitoa mada kama Mkufunzi kwenye Kongamano la Jukwaa la Walimu makada wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Songwe.
Magarinja aliwataka Walimu waendelee kudumisha Mahusiano mema kati ya Chama na Serikali Kwa lengo la kuleta ustawi,utulivu ndani ya nchi pamoja na kusimamia Itikadi za Chama Cha Mapinduzi ikiwemo Ujamaa na kujitegemea kwani ndiyo msingi Mkuu unaowafanya wanaCCM kuwa wamoja bila kubaguana.
Magarinja amesema CCM itaendelea kufuata Itikadi zake za Ujamaa na kujitegemea kwa kuwa zimekuwa mhimili mkubwa wa kuwezesha WanaCCM kuwa wamoja katika na kufanikisha ushindi wa CCM kwenye chaguzi mbalimbali kwani ushindi wa CCM unatokana na namna Makada wake wanavyo kuwa wamoja na kujitoa kupitia rasilimali zao kwa maslahi mapana ya Chama Cha Mapinduzi
Post A Comment: