Na Fredy Mgunda, Songwe.
Zaidi ya walimu 500 Mkoani Songwe wamepewe elimu ya namna ya kutafuta kura za chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani 2025 nchi nzima.
Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo katibu wa siasa, uenezi na mafunzo kutoka mkoa wa Iringa, MWL Joseph Ryata aliwataka Makada hao kuhakikisha wanaenda kutoa elimu kwa wananchi wajitokeze kujiandikisha kwenye vitambulisho vya mpiga kura.
MWL Ryata alisema ili CCM ishinde kwa kishindo inahitaji mtaji mkubwa wa wapiga kura na jukumu hilo wanapewa walimu Makada wa CCM mkoa wa Songwe.
Alisema chama cha Mapinduzi (CCM) kina njia na msingi yake ya kupata ushindi hivyo ni vyema Makada hao wakaelewa namna gani ya kuwa tayari kuzitafuta kura za CCM katika uchaguzi ujao.
MWL Ryata alisema walimu wamekuwa wana ushawishi mkubwa katika kila jambo huko wanakoishi na jamii watumie nafasi na nguvu waliyonayo kuhakikisha wananchi wakiandikisha kwa wingi na CCM inashinda kwa kishindo
Post A Comment: