Wadau wanaotekeleza afua za uelimishaji kuhusu masuala mbalimbali ya afya wamesema wataendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa afua mbalimbali za afya.

Wakizungumza tarehe 5, Novemba, 2024 katika Kikao cha Wadau wa Elimu ya Afya chenye lengo la kuimarisha afua mbalimbali za afya, baadhi ya wadau hao wamesema kuwa lengo la kuwa na miradi ya elimu ya afya ni katika kuhakikisha jamii inakuwa na mabadiliko chanya na kuwa na afya njema.

“Sisi tupo tayari kuendelea kushirikiana na Serikali, na tunapokuwa tunatekeleza miradi ya afya mfano kwenye suala la utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, suala la lishe, eneo la ustawi wa jamii, elimu ya afya kuhusu magonjwa ya mlipuko,afya kwa vijana tunashukuru kwa kuendelea kushirikiana na serikali”amesema mmoja wa wadau.

Meneja Mradi kutoka Pathfinder Sitti Shio amesema mfumo wa M-mama umerahisisha huduma za rufaa kwa mama mjamzito na mtoto mchanga kwa kupiga namba 115 bila malipo .

Naye Mratibu wa Wadau na Mratibu wa hamasa wa M-mama kutoka Wizara ya Afya Simon Nzilibili amesema mfumo wa M-mama umekuwa na mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya mama mjamzito na mtoto mchanga ambapo kila halmashauri inatumia mfumo huu 

“Kila halmashauri inatumia mfumo huu wa M-mama na Wizara mtambuka kama vile, Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Wadau zimekuwa bega kwa bega katika kuhakikisha mfumo wa M-mama unatekelezwa “amesema.

Akizungumzia kuhusiana na mifumo ya afya inavyoweza kuleta ufanisi Afisa kutoka Mpango wa Taifa wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii, Wizara ya Afya Bahati Mwailafu amesema mifumo ya kidijitali ya afya ina ufanisi mkubwa katika uimarishaji wa huduma za afya huku akisema kuna umuhimu mkubwa Mpango wa Taifa wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii kuhusishwa kila afua ya afya .















Share To:

Post A Comment: