Na Denis Chambi, Tanga.

MKUU wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani ameeleza kuwa ofisi yake  inaendelea kufwatilia mchakato wa ufufuaji wa viwanda vilivyofungwa muda mrefu huku akiwataka wawekezaji walioshindwa kuviendelea wavirejeshe serikalini ili kurudisha hadhi ya mkoa huo kama ulivyokuwa .

Balozi Dkt Buriani ameyasema hayo Leo wakati wa h Dua maalumu ya kuliombea amani Taifa  iliyowakusanya wananchi wa mkoa wa Tanga pamoja na viongozi wa madhehebu ikiambatana na  kumuimbea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa kutokana na miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa Mkoani Tanga ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Bomba la Mafuta linalotoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga Tanzania pamoja na ujenzi wa Barabara ya kutoka Tanga Pangani hadi Bagamoyo Mkoa huo unazidi kufungaka kimaendeleo hivyo uwepo wa viwanda hivyo utatatua
 changamoto ya ajira kwa wananchi.

"Bado tunaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji, Tanga ulikuwa ni Mkoa wa viwanda lakini baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki viwanda vingi viliweza kusimama na katika ubinafsishaji hatukupata bahati ya kupata wawekezaji makini ambao waliokuwa na nia hasa  ya kuendelea vile viwanda"

"Sisi kama ofisi ya mkoa tunaendelea kuwafatilia  wale ambao wamenunua vile viwanda  kuona kwamba ama wanaviendeleza au vinarudi serikalini bado wananchi wa Tanga wanahitaji ajira ambayo sasa imekuwa ni changamoto hususani kwa vijana tunataka tuwekeze mazingira mazuri ya vijana kujiajiri" alisema Dkt Buriani.

Akizungumza Mwenyekiti wa Amani Mkoa wa Tanga Sheikh Juma Luuuchu  alisema kuwa ipo kila sababu ya Watanzania kumshukuru Mungu kwa Neema na baraka zake kuendelea   kuijalia  Tanzania amani kwa mwaka 2024 huku wakimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu kwa uongozi wake mahili.

"Kusudio kubwa la kukutana ni kumshukuru Mungu  kwa Neema mbalimbali anazotujalia wananchi wa Tanzania na kwa upekee Mkoa wetu wa Tanga tunamshukuru sana Mungu kwa kutujalia na  kutupatia kiongozi mpole msikivu na mwenye upendo kwa watu anaowaongoza  ambaye ni Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan  

"Lakini pia tunaiombea nchi yetu amani na utulivu tunamshukuru Mungu kutujalia amani kwa mwaka mzima , viongozi wa dini tuendelee kuombea nchi kuwalea watoto wetu katika maadili yaliyo mema kila mmoja ahakikishe amani unapatikana kuanzia majumbani" alisema Sheikh Luwuchu.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Abdurahman Shiloow ametumia jukwaa hilo kumpongeza Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani kufwatia tamasha la Tanga festival lililofanyika hivi karibu ambalo lilibebwa na tamaduni , vyakula vya asili pamoja na michezo mbalimbali.




Share To:

Post A Comment: