Na Denis Chambi, Tanga.
JUMUIYA ya wataalamu wa Miamba Tanzania 'TGS' Wameiomba Serikali kuanzishwa kwa bodi ya usajili ya wanajiojisayansi ' TGRB' ambayo itasaidia kuzifanya taaluma hiyo kuwa rasmi na kutambulika kitaifa na kimataifa.
Ombi hilo limetolewa na Rais wa jumuia hiyo Dkt Elisante Mshiu wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa mwaka 2024 Mkoani Tanga wa wanajumuia hao pamoja wadau kutoka nje ya nchi zikiwemo Uingereza, Burundi na Uganda ambapo ameeleza kuwa kuundwa kwa bodi hiyo sii tu kuwawezesha kutambulika kimataifa bali wataweza kuliongezea Taifa pato kupitia fedha za kigeni.
"Ili kuweza kufanya kazi hii vizuri na kwa kiwango cha hali ya juu bodi ya usajili ya wanajiolojisayansi ni muhimu sana, tunatambua juhudi za Serikali na zaidi kupitia wizara ya madini, ili tuweze kufanikiwa tunaona kabisa kikwazo kikubwa cha ndoto zetu ambacho kinaweza kitukwamisha ni kitokuwepo kwa bodi hii ya usajili ya 'TGRB' bodi hii itasaidia kuleta matokeo chanya ya kuaminika ya kazi za tafiti na mwishowe matokeo yake ni ugunduzi wa migodi mipya" alisema Dkt. Mshiu.
"Baada ya kuwa na bodi hii tafiti za uhakika zitafanyika na kusambaa sio kwa vyombo vya Serikali bali hata na kwa sekta binafsi na hata kupitia kwa wachimbaji wadogo" aliongeza
Aidha Dkt Mshiu amebainisha kuwa bado Tanzania katika sekta ya Madini ina uhaba wa wanajiolojia wanaotambulika kimataifa kwani mpaka sasa ni wanne pekee wanaotambulika hali ambayo inayalazimu makampuni ya ndani kuwatumia wajiologia kutoka nje ya nchi ambao hulipwa fedha nyingi hivyo kuwepo kwa bodi hiyo kutawasaidia wazawa kuweza kutumbulika katika masoko ya ndani na nje na hatimaye kuwezesha kuongezeka kwa Pato la Taifa.
"Bodi hii itasaidia kuongeza utambuzi wa kazi za wajiolojia kimataifa na hivyo kuweza kuaminika katika masoko ya mitaji ya Dunia ambapo mpaka sasa ni ripoti chache za wajiolojia zinatambulika katika masoko hayo lakini kuwepo kwa bodi hii itakuwa ni ngazi kwa wajiolojia wote nchini Tanzania kuweza kutambulika"
"Kuwepo kwa bodi hii itasaidia pia kwa wanajiolojia kufanya kazi kimataifa na kuleta fedha hapa nchini kwa viwango vya itendaji wake kwa sasa wanajiolojia wanaotambulika kimataifa hawazidi wanne lakini tupo zaidi ya elfu nne bodi hii ndio suluhisho la kuwawezesha wajiolojia kutambulika"
Kukosekana kwa wajiolojia wa ndani tunapongeza gharama kubwa za wajiolojia kutoka nje ambao wanao utambuzi wa kimataifa katika kazi zao hivyo wanalipwa gharama kubwa" alisisitiza Dkt Mshiu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Tanga , katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji wa huo Amidius Kasunzu amewapongeza wanajiosayansi kwa kazi wanazozifanya katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo wamewezesha Tanzania kutambulika kimataifa kupitia ugunduzi wa rasilimali mbalimbali ikiwemo Madini na gesi asilia.
"Wanajiologia wanafanya kazi kubwa sana, migodi mingi ambayo tunayo Tanzania ni matokeo ya utaalamu unaofanywa na wanqsayansi Hawa katika tafiti zao kada hii inagusa Kila nyanya ya wananchi wa Tanzania
Katika Mkoa wa Tanga wanajiosayansi wamewezesha kupatikana kwa Madini mbalimbali Mkoa wa Tanga niwapongeze sana"
Akifungua mkutano huo wa mwaka kwa niaba ya waziri wa Madini , naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo Msafiri Mbibo amesema kuwa Serikali ipo mbioni kufungua masoko mapya ya madini ambayo yatawawezeaha wachimbaji wakubwa na wadogo kupata kipato zaidi na hatimaye kuweza kuchangia pato la Taifa.
"Mbali na makusanyo na ajira, tumeshuhudia hatua za kimkakati zinazochukuliwa na Serikali ili kusafirisha madini ghafi; kuboreshwa kwa mazingira ya wachimbaji zipo hatua
zilizochukuliwa na Serikali zenye lengo la kuimarisha sekta ya madini kwa kunzishwa kwa kwa masoko na vituo vya ununuzi wa madini nchini; utekelezaji wa
for Brighter Tomorrow (MBT); na usimamizi makini wa utekelezaji
ajenda ya kuongeza thamani ya madini ndani ya nchi" alisema Mabibo.
Aidha amesema kuwa sekta ya madini hapa nchini imeendelea kuimarika ambapo katika makusanyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 zimeweza kukusanya shilingi Bilion 753 huku kwa upande wa Madini ikiongezeka kutoka na kufikia Bilion 161 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwa ni sawa na asilimia 368.
Ameongeza kuwa mpango wa Taifa juu kuhama kutoka nishati chagu kwenda kwenye nishati safi ni wajibu wa kila mtanzania kutekeleza ikiwa pia ni mpango wa kimataifa hivyo kuendelea kuwahimiza wadau mbalimbali kuendana na mpango huo wa Taifa.
"Kwa habari ya kuhama kutoka matumizi ya nishati chafu kwenda nishati safi yani energy transition, ni dhahiri kuwa ajenda hii waTatuwa Maendeleo wa Taifa waMiaka Mitano 2021/22 -2025/26 na mipango mingine ya kikanda na kimataifa kama vile imeshika hatamu duniani hasa kutokana na mabadiliko ya tabia dira ya Afrika Mashariki 2050, Ajenda 2063: Afrika Tunayoitaka; na
nchi yanayoshuhudiwa. Suala la matumizi ya nishati safi limewekwa bayana katika mipango ya kitaifa kama vile Mpango Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030"alisema
Mkutano huo ambao unaofanyika Mkoani Tanga kwa mwaka 2024 umebebwa na kauli mbiu ya "Kutumia utajiri wa Madini Tanzania kwa maendeleo endelevu na kuhama kutoka nishati chagu kutumia nishati safi" huku ukitarajiwa kuhitimishwa December 6,2024.
Post A Comment: