Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwa miongoni mwa Mawaziri wa Kisekta walioshiriki Jukwaa la Biashara na Uwekezaji lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Artabia kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIA na Kituo cha kuendeleza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), lililofanyika makao Makuu ya Chemba ya Wafanyabiashara yalipo Riyadh nchini Oman, ambapo Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Jukwaa hilo alikuwa waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo.

Jukwaa hilo limewaleta pamoja wafanyabiashara wa Tanzania na Saudi Arabia, ambapo kwa siku kadhaa, watapata nafasi ya kujadiliana kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana katika nchi hizo mbili ili kukuza biashara na uwekezaji, hatua ambayo lengo lake ni kuinua na kukuza zaidi uchumi wa nchi hizo mbili.

Akifungua Jukwaa hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, alisema kuwa licha ya ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo kudumu kwa zaidi ya miaka 40, kiwango cha biashara (mauzo) kati ya Tanzania na Saudi Arabia kiko chini na kimekuwa kikiunufaisha upande mmoja wa Saudi Arabia, ambapo wakati mauzo ya nje ya Saudi Arabia nchini Tanzania yakifikia dola za marekani bilioni 52.3, Tanzania imeiuzia nchi hiyo bidhaa zenye thamani ya dola milioni 12.3 pekee.

Alitoa wito kwa kampuni za Saudi Arabia kwa kushirikiana na wenzao wa Tanzania, kuongeza uwekezaji na kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili kwa kutumia fursa za kiuchumi na mazingira bora ya uwekezaji yaliyopo hivi sasa nchini Tanzania kuwekeza mitaji ili kunufaika na soko kubwa linalipatikana nchini Tanzania na nchi jirani hususan katika sekta za kilimo, usindikaji bidhaa za kilimo, nishati ya kijani, uchumi wa buluu, madini, mafuta na gesi pamoja na masuala ya kidigitali.
Share To:

Post A Comment: