📌Lengo ni kuhakikisha asilimia 75 ya watanzania wanapata umeme wa kutosha,nafuu na uhakika na usio na athari za mazingira ifikapo 2030

📌Asema Tanzania imejipanga kupokea Marais 15 kujadili utekelezaji wa. Ajenda ya kuwafikia Waafrika  milioni  300 kupata  umeme


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mha. Felchesmi Mramba amesema Tanzania imejipanga kuhakikisha mpango wa kuwafikia wananchi kwenye huduma ya umeme unatekelezwa na unapewa kipaumbele na watanzania wapatao asilimia 75 wanafikiwa na nishati hiyo kwa uhakika,gharama nafuu, na usio na athari za mazingira  ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni mpango wa utekelezaji kwa nchi za Afrika kupitia mpango ujulikanao kama mission 300.

Mha. Mramba amesema hayo leo 13 Desemba,2024 ,wakati wa mkutano na wadau mbalimbali kwenye sekta ya nishati, wenye lengo la kujadili Azimio la nchi ya Tanzania kufikia lengo la kuwa na upatikanaji wa umeme wa uhakika ili makubaliano hayo yawekwe saini kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, unaotarajia kufanyika mwanzoni mwa mwaka ujao nchini Tanzania.

‘’Niwahakikishie tumejipanga na tuko tayari kuhakikisha watanzania wanapata umeme kupitia miradi mbalimbali iliyoainishwa kwenye ajenda ya nchi kwa uhakika na kwa gharama nafuu ili kufikia lengo walilojiwekea’’ Alisema Mha Mramba.

Awali akitoa wasilisho la rasimu ya azimio la nchi ya Tanzania , mwakilishi kutoka wizara ya Nishati Mha. John Mageni amesema ,miongoni mwa miradi iliiyopewa kipaumbele ni pamoja na ile ya gridi imara, uboreshaji wa miundombinu ya kusambaza umeme  pamoja na maeneo ya  uzalishaji umeme.

Mkutano huo uliwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya Nishati benki ya dunia,Benki ya maendeleo ya Afrika  na wawakikishi kutoka sekta binafsi, mabalozi ili watoe maoni kwa ajili ya maboresho kwenye ajenda ya Tanzania.







Share To:

Post A Comment: