Na Oscar Assenga,
TAMASHA Kubwa la Same Utalii Festival Season 2 linatarajiwa kufanyika Desemba 20 hadi 22 mwaka huu katika wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro ambalo limeidhinishwa kufanyika kila mwaka lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu kuhamasisha utalii nchini.
Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni alisema kwamba maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na litatanguliwa na lingine Desemba 17 hadi 19 kutakuwa na matukio yatakayotanguliwa tamasha hilo.
Aliyataja matukio ambayo yatatangulia kabla ya kufanyika kwa Tamasha hilo ni Utalii wa Matibabu (Tourisim Clinic) ambapo wananchi watapata matibabu bure ya utalii na kutakuwepo na madaktari ambao watachunguzi wananchi wenye changamoto za magonjwa mbalimbali .
“Hii itafanyika kwa ajili ya wananchi wa Same na hata wale ambao watakuwa wamewahi mapema kwa ajili ya tamasha hili nao watanufaika na huduma hiyo wakati wakisubiri kuanza kwake”alisema
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba katika kuelekea Tamasha hilo Desema 18 mwaka huu kutakuwa na treni itakuwa inatokea Dar kwenda wilaya ya Same kwa ajili ya utalii itakuwa imebeba watalii wa kitanzania na wengine kutoka nje ambapo itaanza safari zake Desemba 18 jioni na watafika Desemba 19 asubuhi.
“Lakini pia kutakuwa na mabehewa manne kwa watalii wanaokuja ,behewa la nyama choma,vinjwaji na michezo aina mbalimbali kwa watoto ili watoto wasiboreke wawe na eneo lao la michezo na kutakuwa na mabehewa la mziki mpaka watakapofika same Desema 19 tayari kuanzia utalii 20 hadi 22”Alisema
Aidha alisema wameona utalii waubadilishe kidogo na wapo watakaokuja kwa njia ya magari ambapo Desema 20 kutakuwa na uzinduzi rasmi wa tamasha wataenda kutalii kwenye hifadhi ya Mkombazi na jioni watarudi kutakuwa na mkesha kwa ajili ya watalii mbalimbali kupata burudani kutoka kwa wanamuziki mbalimbali watatumbuiza .
Mkuu huyo wa wilaya alisema katika kunogesha Tamasha hilo Desema 21 mwaka huu idadi ya watu wameongezeka kutoka 2000 kipindi kilichopita na wanatarajiwa kuongezeka kufikia watu 20,000 kwa sababu wameongeza kipengen za marathon.
Alisema katika watu watakimbia kuanzia Kilomita 21,Kilomita 10 na Kilomita 5 na wengine watakwenda kutalii mlima Kidenge ambao ni mlima mzuri unaofanana na ukuta mmoja uliojengwa nchini china upo wilayani humo ambao ulifufuliwa hivi karibuni na wizara wameridhia uwe kivutio cha utalii.
Akizungumzia mlima huo alisema ni mzuri na unakona nzuri na Rais Dkt Samia Suluhu amewajengea barabara nzuri ili kuwezesha watalii kuweza kufika bila kuwepo kwa changamoto huku akitaja kivutio kingine kuwa ni upepo mkali na mlima shengena uliopo kwenye Hifadhi ya Msitu wa Chome una vivutio vingi vya utalii kuna ndege ambao hawapatikana duniani ilisopokuwa huko shengena.
Alisema pia kuna chura ambaye hapatikana sehemu yoyote duniani na watu wataendelea na burudani ya mziki kutoka kwa wasani mbalimbali ambao watatumbuiza kwenye siku hiyo niwakaribishe watanzania wote kwa ujumla
“lakini pia kutakuwa na mabanda mbalimbali ya maonesho yataaandaliwa kwa ajili ya tamasha hilo litafanyikia same mjini na Marathon zitaanza hapo na kutakuwa na bidhaa mbalimbali zitakazonyeshwa na watalii”Alisema
“Lengo la Tamasha hili ni kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu tunavyofahamu aliweza kutangaza vivutio vya utalii nchini na kuweza kuingiza fedha za kigeni kupita Filamu ya The Rayal Tour sisi hapa Same tumebaini vipo vivutio vya utalii ambavyo havijatangazwa na hivyo kutumia nafasi hiyo kuzitangaza”Alisema
Hata hivyo alisema lengo pia ni wananchi wa wilaya ya Same wainuke kuichumi kupitia Same Utalii Festivali na hivyo kuinua kipato cha wajasiriamali,wamiliki wa hoteli,mama ntilie ,bodaboda na kuna bidhaa zinazotokana na utalii uliopo same nao wenyewe watapata fedha na hivyo kuinuka kiuchumi.
“Wananchi wamehamasika sana baada ya kufanyika lile tamasha la kwanza ambalo lilifanyika na hivyo kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wana nchi na kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya utalii kuweka Same kwenye Mahoteli muhimu “Alisema
Akizungumza namna tamasha hilo lilivyoongeza idadi ya utalii alisema kabla wajaanza Same Utalii Festival takwimu zilionyesha katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi idadi ya watalii walikuwa kati ya 3,000 hadi 7,000 kwa mwaka.
Alisema baada ya tamasha kufanyika kwa mujibu wa takwimu za Hifadhi hiyo watalii wameongezaka kutoka 3,000 hadi 7,000 hadi kufikia elfu 9,000 na wamebaini lazima kuwepo na hotel nyingi za kutosha hivyo kuwahamaisha wawekezaji kuwekeza kwenye wilaya hiyo ili huku akieleza hotel mbili zimejengwa kupitia uhamasishaji huo eneo la Shengena na jengine kwenye lango la hifadhi ya Mkomazi.
Post A Comment: