Wananchi wa wilaya ya Newala, Tandahimba na Mtwara hawatakaa wamsahau Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na mradi wa maji wa Makonde ambapo Serikali kwa kushirikiana na Shirika la CI Imate Resilient Infrastructure Development Facility (CRIDF) wameamua kuboresha uzalishaji na kuboresha huduma ya maji ya Makonde kupitia chanzo cha Mitema.
Mradi huo ni mkongwe ambapo tangu ujengwe mwaka 1984 kwa ufadhili wa Serikali ya Finland haujawahi kufanyiwa ukarabati ambapo Rais Samia amemulika mradi huo na fedha Kiasi Tsh. Bilioni 84.7 kutumika kuuboresha na Watu zaidi ya 670,984 kunufaika.
Mradi utakapokamilika utakuwa na uwezo kuzalisha Lita za ujazo wa maji milioni 26 ambayo ni zaidi ya mahitaji ya maji kwa miaka 15 ijayo. Nani kama Rais Samia? Jibu ni "Hakuna"
Maboresho hayo yatahusisha uchimbaji wa visima sita virefu, ujenzi wa matanki makubwa ya kuhifadhia maji na usambazaji wa maji kwenye Halmashauri nne za wilaya 3.
Kwa sasa Watu wanaopata maji safi na salama ni 335,354 sawa na asilimia 62 huku mahitaji ni Lita 23,000,000 kwa sasa uzalishaji ni wastani wa Lita 10,800 kwa siku huku mapungufu yakiwa ni Lita 12,200,000 ambapo mradi ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha hadi Lita 36,284 na hivyo kukidhi mahitaji ya Wananchi wapatao 805,526 wanaoishi katika Halmashauri ya wilaya ya Newala, Halmashauri ya mji Newala, wilaya ya Tandahimba na Halmashauri ya mji Nanyamba. Hakika upele umempata mkunaji, Rais Samia.
Narudia tena kumpongeza Rais Samia kwa mradi huu wa kimkakati wa kuboresha maji kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara, hakika amekata kiu na amewatua ndoo kichwani akina Mama. Heko Rais Samia!
Post A Comment: