Denis Chambi, Tanga.
JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga kupitia oparesheni yake maalumu ya usalama barabarani kwa muda wa siku 15 limefanikiwa kukusanya fedha tathlimu Kisi cha shilingi Milioni mia moja kumi na tisa lakini sita na ishirini na Tano (119,625) ambazo ni tozo za papo kwa papo kutokana na makosa mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi amesema kuwa opareshini hiyo ambayo ilifanyika kwa siku 15 imewabaini madereva 15 wakifanya makosa mbalimbali ambapo wamepokonywa leseni zao.
Kamanda Mchunguzi ameongeza kuwa katika oparesheni hiyo magari 10 yasiyofaa kutembea barabarani yamekamatwa na kuondolewa namba za usajili huku Jeshi hilo likitoa rai kwa wamiliki wa vyombo hivyo kuvirekebisha ikiwa ni takwa la kisheria za barabarani.
"Katika juhudi za kudhibiti ajali za barabarani na kuhakikisha usalama wa wananchi Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limefanya oparesheni maalumu iliyoanza tarehe 15 hadi 30 Disember 2024 ambapo madereva 15 wamefungiwa leseni zao za udereva kwa makosa mbalimbali ya barabarani , makosa 404 ya usalama barabarani yameripotiwa na kiasi cha shilingi 119,625,000 kimekusanywa kama tozo za papo kwa papo"
"Katika oparesheni hiyo magari 10 yasiyofaa kutembea barabarani yalikamatwa na namba za usajili ziliondolewa huku wamiliki wa magari hayo wakitakiwa kuyarekebisha kabla ya kuruhusiwa kurudi tena barabarani" amesema Kamanda Mchunguzi.
Aidha kamanda huyo ametoa Rai kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kupunguza ajali za barabarani hususani kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambazo zimekuwa zikighalimu maisha ya watu na mali zao akiwataka wananchi kusherehekea sikuu za mwaka mpya kwa amani na kusisitiza kuwa Jeshi halitomvumilia yeyote atakaye kiuka sheria.
"Ili kuhakikisha kuwa Mkoa wetu wa Tanga unaendelea kuwa salama mikakati ya ulinzi imeimarishwa kwa kushirikiana na wananchi pamoja na viongozi wa kijamii ili kuhakikisha amani inatawala kwenye maeneo muhimu Barabara kuu, nyumba za ibada , kumbi za starehe , fukwe za bahari na sehemu zote zenye mkusanyiko ya watu" alisema.
Post A Comment: