Na Denis Chambi, Tanga.

BAADA ya kuthibitishwa na wajumbe zaidi ya 235 kuwa ndiye  mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union 'Wagosi wa kaya'  katika  uchaguzi na mkutano mkuu Hassan Muhsin ameitaja falsafa yake ya Umoja kuwa  kipaumbele chake  kikubwa itakayosaidia  kuwavutia wawekezaji  na wadhamini watakaoiwezesha timu hiyo kufanya vizuri kwenye ligi kuu na michuano ya kimataifa.


Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo Muhsin amewashukuru wajumbe waliohudhuria mkutano huo akiwataka kuvunja makundi na kuimariaha umoja  na mshikamano  ili kuweza kuyafikia malengo ambayo watayaweka kwa pamoja kwa maslahi mapana ya klabu.

"Tutajitahidi kuwekeza katika kwa wafadhili tunaamini kuwa wafadhili hawawezi kwenda sehemu ambayo haijatulia  lazima tuwe na umoja tukitulia tunao uwezo wa kupata wafadhili miaka zaidi ya 10 iliyopita Coastal Union hatukuwepo na mfadhili hata mmoja  lakini sasa hivi angalau tuna wafadhili wawili watatu tutajipanga kwa pamoja  ili kuimarisha ushirikiano na wawekezaji na kutafuta vyanzo vingine vya mapato" alisema Muhsin.

Alisema atahakikisha anaendelea kulisimamia soka la vijana jukumu ambalo alikuwa nalo tangu akiwa makamu mwenyekiti ambapo amewezesha kuwaibua wachezaji wanofanya vizuri  kwenye ligi kuu katika timu mbaalimbali akiwemo Bakari Nondo Mwanyeto aliyepo Yanga kwa sasa , Charles Semfuko, Ramadhani Chuma Miraji wote wakiwa Coastal Union. 

"Tumekuwa tulitegemea sana vijana ambao tunawaibua sisi wenyewe  hii ni sehemu ambayo nilikuwa naishighulikia mimi mwenyewe zaidi ya miaka 6 nilikuwa ni mlezi na kwa kuanzia  tumejipanga pia na timu za wanawake  ambayo ni kama tulikuwa tumeiacha  hatukuwa na kipaumbele nayo sana" aliongeza

Aidha alisema bado Klabu hiyo inahitaji wanachama wengi zaidi ya waliopo kwa sasa kulinganisha na ukubwa walionao hivyo kutangaza kutanua wigo wa kuongeza idadi  yao ndani na nje ya Tanzania ambao kwa kulipia ada zao za uwanchama watachangia kwa kiasi kikubwa maendeo ya klabu.

"Tuna tatizo la kuwa na wanachama hai wachache  katika kumbukumbu zetu tuna wanachama zaidi ya 700 lakini waliopo hai ni 300  tunataka tuliboreshe hili tuweke utaratibu mzuri wa kuwafanya watu waipende klabu yao tunakwenda pia kuongeza wanachama nje ya nchi yetu sio Tanga tu" alisema

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Steven Mguto ameutaka uongozi mpya kuhakikisha hautoi mwanya kwa wanachama wasiolipa ada kuwapasua vichwa pale wanapohitaji kupiga hatua mbele jambo ambalo amelitaja kuwa linavitesa vilabu vyote vya wanachama hapa Tanzania ikiwemo Simba na Yanga. 

"Klabu zinazotegemea wanachama zina shida nyingi na sio kwa Coastal Union pekee hata kwa Simba na Yanga wapo wanachama wapo tu na hawalipi ada wala kufwatipia mambo ya klabu sasa tunataka uongozi unaokuja ukomeshe mtindo wa  wanachama kulipiwa ada  zao na ndio hao wenye maneno ya  kudhoofisha klabu" alisema Mguto

Muhsin alitangazwa kuwa mwenyekiti wa Klabu hiyo akiwa ndiye mgombea pekee kwa nafasi hiyo aliyekidhi vigezo  ambapo pia amepewa kwa  Mamlaka aliyopewa amemteua Dkt. Fungo Ally Fungo kuwa mamaku mwenyekiti huku wajumbe saba wakutano Mkuu wakichaguliwa kwa kupigiwa kura.

Wajumbe Saba waliochaguliwa katika uchaguzi huo kati ya 15 waliowania nafasi hizo  ni Nasoro Mohammed  akipata kura 171 ,  Ally Shechonge (169) Bakari Mohammed (142), Abdallah Zuberi (136) Hussein Abdallah (133)  pamoja na Bakari Fumbwe (112) Emmanuel Mchechu (140).
 
Share To:

Post A Comment: