Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasuku mkoani Kigoma Teresia Mtewele akifanya usafi kwenye hospitali ya Mlimani Kasulu mji
Baadhi ya viongozi wakiwa na vifaa vya kufanyia usafi tayari kwa zoezi la usafi
Baadhi ya viongozi wakiwa mstari wa mbele kabisa kufanya usafi
Na Fredy Mgunda, Kasulu,Kigoma.
Uongozi wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wameadhimisha sherehe za siku ya Uhuru kwa Kufanya Usafi katika maeneo mbalimbali yanayozunguka wilaya hiyo yakiwemo maeneo ya Hospitali.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo,
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasuku mkoani Kigoma Teresia Mtewele amewataka wananchi kuendeleza Utamaduni wa kufanya Usafi wa mazingira ili kudhibiti magonjwa ya milipuko na kudumisha afya ya kila mwananchi.
Mtewele amewataka wataalamu wa Afya kuendelea kutoa Elimu ya Usafi wa mazingira katika jamii kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji na Vitongoji.
"Zoezi hili la Usafi lisiishie leo tu bali uwe utamaduni wetu na kama mnavyojua kumekuwa na changamoto ya mlipuko wa magonjwa hivyo kufanya usafi ndio njia sahihi ya kuepukana na magonjwa hayo.
Mtewele amewataka wananchi kuendelea Umoja, amani na mshikamano wa Taifa la Tanzania kwa vizazi vijavyo.
Post A Comment: