Na,Jusline Marco;Arusha
Mkutano wa pili wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika unaoendelea jijini Arusha Arusha umekutanisha wadau mbalimbali katika maonesho yaliyoambana na mkutano huo kwa lengo la kutoa elimu na huduma kwa wadau wa sekta ya Uhasibu na Ukaguzi wa ndani.
Akizumgumza katika maonesho hayo Mkuu wa Masoko na Mauzo kutoka APC Hotel and Conference Centre Michael Frank Mwakifuna amesema ushiriki wako kwenye maonesho hayo katika mkutano huo ni ili kuitangaza hoteli hiyo kwa wadau mbalimbali nchini na nje ya nchi.
"Tupo jijini Arusha katika mkutano huu ili kuitangaza hoteli yetu na kuwapa nafasi watu kutujua zaidi na kufahamu uwezo Wetu."Alisema Ndg.Michael Frank Mwakifuna Mkuu wa Masoko na Mauzo kutoka APC Hoteli
Amesema Hotel hiyo yenye miaka saba tangu kuanzishwa kwake, ina uwezo wa kuchukuwa idadi ya watu tofauti na kumbi zaidi ya kumi ambayo pia iko katika eneo lenye ukubwa wa heka 13 iliyojumuia viwanja mbalimbali vya michezo na inamilikiwa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania NBAA.
Ameongeza kuwa lengo kubwa la kuanzisha hoteli hiyo ni kusaidia katika shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na NBAA pamoja na sekta ya tofautitofauti ili kuweza kukuza maendeleo ya nchi.
Sambamba na hayo amesema hatua hiyo inaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutangaza Utalii wa Mikutano na Biashara kupitia sekta ya Utalii hivyo ujio huo jijini Arusha utawawezesha katika uungaji mkono kauli hiyo na kuingia kwenye mnyororo wa thamani.
Post A Comment: