Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amezindua Kikundi cha VICOBA Women Power For Development kilichopo jijini Dar es Salaam chenye jumla ya wanachama thelathini wenye lengo la kuwezeshana kiuchumi pia kuisaidia jamii hususani vijana na wanawake.
Mkurugenzi wa Kikundi hicho Violet Konyani amesema matarajio ni kuanzisha Saccos itakayowakwamua zaidi kiuchumi.
Mbali ya uzinduzi wa kiikundi hicho Mkurugenzi wa Taasisi hiyo alitumia fursa ya kugawa tuzo kwa Wanawake wanaofanya vizuri katika sekta mbalimbali akiwemo Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi kutokana na utendaji mzuri wa majukumu ya Serikali pamoja na juhudi za kuwapigania wanawake nchini bila kujali itikadi zao.
Akitoa hotuba yake Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amehimiza mshikamano pia akiwataka kutumia fursa ya mikopo ya Wanawake inayotolewa na Serikali.
Katika ujenzi wa ofisi ya kikundi ameahidi kuwasiliana na Wakurugenzi wa Halmashauri ili wapate eneo la kufanyia shughuli zao.
Post A Comment: