Na Mwandishi Wetu,BUKOBA.

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia CCM anawakilisha NGOs Tanzania Bara Neema Lugangira amelazimika kuingilia kati tukio la kubakwa mwa mtoto wa miaka 9 wilaya ya Bukoba na kuzuia jaribio la kumtorosha mtoto huyo. 


Akizungumza namna alivyopata taarifa kutoka kwa mwananchu kuhusu tukio hilo baya la ubakaji kwa binti huyo mdogo wa miaka 9, Mbunge Neema alisema kwamba alisema kwamba tukio hilo lililotokea Desemba 8 mwaka huu ambapo alipokea simu Desemba 17 kutoka  kwa mwananchi kutoka kata ya  katika kuongea naye mzee huyo alimueleza kuhusu uwepo wa mtoto wa kike wa miaka 9 aliebakwa na kuharibiwa.

Alisema kwamba mkazi huyo alimueleza tukio hilo lilitokea Desemba 8 mwaka huu na baada ya jitihada za wananchi kwenye mtaa bibi wa mtoto akaenda kutoa taarifa Kituo cha Afya ili mtoto apate huduma na baadae kwenda Polisi.

Mzee huyo alimweleza Mbunge Lugangira kuwa kuna jitihada kwamba mtuhumiwa anaweza kutoka kwa dhamana na mtoto aliyefanyiwa ukatili huo atoroshwe na kimeshaandaliwa kiasi cha fedha.

Kufuatia taarifa hiyo Mbunge Neema aliamua kujiridhisha na taarifa hiyo kisha akawasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima  naye akafanya mawasiliano na OCS ambaye  alifika Kituo cha Polisi Bukoba lakini kwa bahati mbaya yule mtuhumiwa wa ubakaji alikwisha tolewa mchana huo kwa dhamana ambapo ambapo walifika wanaume  wawili kuomba dhamana lakini waliambatana na kiongozi.

“Kwa hakika niwashukuru Mhe DC, RPC, OCD, OCS, Dawati la Jinsia na Ustawi kwa kuchukua hatua kwanza kuhakikisha usalama wa mtoto husika na mtuhumiwa amerudishwa ndani kutokana na mazingira tatanishi” Alisema Mhe Lugangira 

“Nimshukuru pia Waziri wa Mambo ya Ndani nilipompa taarifa hii aliibeba kwa uzito ukubwa na Waziri wa Jamii Dkt Dorothy Gwajima ambaye nilimpa taarifa hii naye alitoa maelekezo nitakapofika Bukoba  niambatane na na Bi Rebeccah Gwambasa, Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa tuende polisi kupata taarifa na tuende kukutana na familia” Alisema  Mbunge Neema 

Alisema walifika Polisi na kwenda kwenye familia kuonana na bibi wa mtoto, mama wa mtoto na familia imerejeshewa imani baada ya mtuhumiwa amerejeshwa na yupo mahabusu.

“Lakini nimesikitishwa sana nikiwa kama Mbunge wa CCM kwa sababu kiongozi aliyeambatana na wale wanaume wawili kwenda kuhakikisha mtuhumiwa anapata dhamani ni kiongozi aliyechaguliwa na wananchi kutoka kwenye Kata ya Kitendaguro na kitendo hicho ni kinyume na CCM na CCM haitaungana na haita kuwa sehemu ya uhalifu na CCM ipo kwenye kusimamia haki na tunamsikia Rais Dkt Samia Suluhu Hassa. anavyopambana kuhakikisha anaimarisha haki na utawala bora mpaka akaunda tume maalumu ya haki jinai iliyotoa mapendekezo kama taifa kuumarisha haki jinai na yamefanyiwa kazi, Alisema Mhe Neema Lugangira

Alisema hivyo haiwezekani wao kama viongozi kuwa sehemu ya kupindisha mchakato wa kisheria na jambo hilo limemsikitisha akitambua kitendo cha kiongozi huyo na tayari taarifa ameifikisha kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera na anaamini Chama kitachukua hatua stahiki. 

“Viongozi kunapokuwa na matukio ya kihalifi ukiwemo ubakaji na ulawiti hatupaswi kushiriki na kutafuta namna ya kuharibu ushahidi wa kesi hiyo na serikali imejipanga kuhakikisha inaimarisha,viongozi wasiwe sehemu ya kukwamisha jitihada zinazofanywa na Jeshi la Polisi “Alisema  

Hata hivyo aliwaomba wazazi wajitahidi kuongea na watoto wao na kuwahimiza maadili na mienendo na wawe wanaongea nao mara kwa mara ili waweze wapesi kutoa taarifa katika familia yoyote itakayokumbana  na ukati kwa watoto.

“Kwa Jeshi la Polisi na viongozi tuhakikishe haki inatendeka na nitoe rai kwa mamlaka husika kusimamia vema mchakato wa kesi hiyo uweze kukamilika ili mtuhumiwa huyo aliyebaka mtoto wa miaka 9 afikishwe mahakamani na sheria ichukue mkondo wake na kama itathibitika achukuliwa hatua kali” Alihitimish Mhe Neema Lugangira.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: