Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Paul Makonda ameandaa Matembezi na Maombi Maalum ya pamoja ya kuombea Mkoa wa Arusha na Taifa la Tanzania siku ya Tarehe 09 Desemba, 2024.
Matembezi yataanza saa 02:00 asubuhi kwenye Mzunguko wa Impala (Round about ya Impala) kuelekea Mzunguko wa Clock Tower (round about ya Clock Tiwer) kupitia barabara ya Sokoine (Uhuru Road) na kupandia Mtaa wa Uswahilini (barabara ya St.Thomas Hospital) na kuishia mzunguko wa Mnara wa Mwenge (Makumbusho ya Azimio la Arusha).
Wote mnakaribishwa, Njoo tuzungumze na Mungu juu ya Mkoa wetu wa Arusha, njoo tuseme na Mungu tukiwa tumebeba pamoja bendera ya Nchi yetu ya Tanzania🙏🏻
Kauli Mbiu "Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara; Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yatu"
Kwaya, Kaswida na waombaji mbalimbali watakuwepo
Usipange kukosa ✍
Post A Comment: