Na Mohamed Ali Kawaida, _Mwenyekiti wa UVCCM Taifa_

Ndugu vijana wenzangu!

Tukiwa tunaanza safari ya mwaka mpya wa 2025, nipende kutumia  fursa hii kuwatakia heri ya mwaka mpya, afya njema, na mafanikio tele. Mwaka mpya ni fursa mpya. Ni ukurasa mwingine wa kitabu cha maisha yetu, kitabu ambacho tunaendelea kukiandika sisi wenyewe kwa bidii na maarifa yetu.

Tunapokabiliana na changamoto mbalimbali, ni muhimu tukumbuke kwamba ushindi wetu haupo katika kushindana na wengine, bali katika juhudi zetu binafsi huku tukiwatakia mema wenzetu. Pia umoja na mshikamano wetu kama vijana ndiyo silaha yetu kubwa ya mafanikio

Katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wangu kama Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), nimeona kwa macho yangu nguvu, uthubutu, na bidii za vijana wa Kitanzania katika kulijenga taifa letu. Japokuwa changamoto zipo, lakini fursa ni nyingi mbele yetu, fursa ambazo tukiweza kuzitumia vizuri  zitabadilisha maisha yetu na kuleta faida katika taifa letu. 

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha hapa tulipo. Nawashukuru pia viongozi wenzangu wa UVCCM kutoka katika ngazi zote taifa hadi matawi na kila mwanachama ambaye amechangia mafanikio yetu.

Vijana wenzangu, taifa letu linahitaji nguvu zetu, mawazo yetu, na maono yetu_. Kama alivyowahi kusema Nelson Mandela, “It always seems impossible until it’s done.” Tusikate tamaa. _Tusirudi nyuma. Kila hatua tunayochukua inachangia kujenga Tanzania yenye haki, maendeleo, na usawa_.

John F. Kennedy aliwahi kusema,

"Ask not what your country can do for you, ask what you can do for your country."

Kauli hii inatufundisha kwamba jukumu letu kama vijana ni zaidi ya kusubiri, bali ni tuna paswa kuchukua hatua leo ili kuleta mabadiliko chanya leo na kesho.

Tunapojipanga kwa mwaka huu mpya wa 2025, ni lazima tuendelee kujitoa kwa bidii katika kazi, elimu, biashara, kilimo, siasa, na shughuli nyingine za uzalishaji. _Kila hatua tunayopiga leo ni msingi wa taifa lenye ustawi, umoja, na heshima kwa vizazi vya leo na  kesho_.

Mwaka 2025 ni mwaka wa ushindi kwa vijana wa Kitanzania pia tukumbuke ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani niwaombe tuzidi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Mpiga Kura na tuendelee kuiombea nchi yetu amani na utulivu, tukiombee Chama chetu Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan

Nawatakia mwaka mpya wenye baraka, maendeleo, na mafanikio makubwa._ Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki Vijana wenzangu.


Ahsanteni Sana.

Wenu,

Mohamed Ali Kawaida

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa

Share To:

Post A Comment: