Mwenyekiti wa ngome ya Vijana wa Chama Cha ACT Wazalendo Abdul Nondo kushoto akizungumza na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohammed Kawaida picha ya maktaba
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha mapinduzi (UVCCM ) Mohamed Kawaida asema ana matumaini jeshi la Polisi litasaidia kupatikana kwa mwenyekiti wa ngome ya Vijana wa Chama Cha ACT Wazalendo Abdul Nondo .
Kawaida ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa X Leo baada ya taarifa za kudaiwa kutekwa kwa Nondo na watu Wasiojulikana.
"Nimepokea taarifa za kupotea kwako @abdulnondo2 nimatumaini yangu jeshi la Polisi @tanpol litatusaidia kwa kufanya kazi yake kwa weledi na kuhakikisha unapatikana na unarudi katika majukumu yako ya kila siku ya kuhakikisha tunaijenga "Mama Tanzania"
Post A Comment: