Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndugu Mohammed Kawaida amesema Kazi ya usafirishaji abiria kwa kutumia Pikipiki maarufu kama Bodaboda sio kazi ya laana kama ambavyo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakidai, akisema Kazi hiyo imeajiri Vijana wengi nchini Tanzania na hivyo kusaidia katika kupunguza tatizo la ajira linaloikabili dunia nzima kwasasa.

Wakati akihutubia Vijana hao wanaojishughulisha na Usafirishaji kwa kutumia Bodaboda kwenye Jimbo la Arusha Mjini wakati wa uzinduzi wa Chama chao cha Ushirika, Kawaida ameitaja sekta hiyo kuwa muhimu kiuchumi, akiwataka kujisimamia kikamilifu na kujiepusha kutumika kisiasa katika kuchafua Viongozi.

Mwenyekiti huyo wa UVCCM katika hotuba yake pia amewakumbusha pia kufuata sheria za usalama barabarani, kufuata taratibu walizojiwekea, kujiepusha na ulevi wakati wa kazi, kuacha matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kushirikiana na kupendana kama Vijana.








Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: