Na Denis Chambi, Tanga 

RAIS wa Shirikisho la soka Tanzania 'TFF' Wales Karia amesisitiza kuwa ni jambo la busara na hekima kuheshimu katiba  inayoviongoza vilabu vyote hapa nchini  vilivyopo chini ya mwamvuli wa Shirikisho hilo akijibu hoja iliyotolewa na viongozi wa Simba na Yanga kutaka yeye aendelee kusalia madarakani  .

Karia  ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano na uchaguzi mkuu wa Klabu ya Coastal Union ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu mwenyekiti wa Klabu ya Simba Murtaza Mangungu pamoja na Rais wa Yanga Hersi Said wakiwa kwenye mkutano wa kawaida wa TFF  uliofanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro walioto hoja ya kutaka Karia aendelee kubaki madarakani wakionyesha kukoshwa na uongozi wake ambao umekuwa na tija  kwa  timu za Taifa  ikiwemo Taifa Stars, timu za vijana na kwa upande wa wanawake kuendelea kufanya vizuri.

Hoja hiyo pia iliungwa mkono  na wajumbe zaidi ya 200 waliohudhuria mkutano Mkuu wa Klabu ya Coastal Union ambapo  mwenyekiti aliyemaliza muda wake Steven Mguto alisema kuwa kwa sasa hakuna anayeweza kuvaa viatu vya Karia  kuliongoza Shirikisho la soka Tanzania 'TFF' hivyo ni vyema Karia kuendelea na nafasi yake.

"Tunampongeza sana Rais wa TFF kwa namna ambavyo analiongoza Shirikisho letu katika kipindi chake chote kumekuwa na mafanikio makubwa kwa Taifa letu timu zetu za Taifa zinaendelea kufanya vizuri tumepata bahati ya kuhodhi michuano ya CAF , na sisi Coastal Union tunaungana na wenzetu wa Klabu za Simba na Yanga kutaka Rais wetu aendelee bado hatujaona ambaye ataweza kumrithi" alisema Mguto.

Akizungumza katika Mkutano huo wa Coastal Union ambapo pia ni mjumbe Rais wa  TFF Wales Karia alisisitiza kuwa yeye ni muumini na  anaiheshimu na kufuata katiba inayowaongoza na pendekezo hilo lisichukuliwe kimihemko kwani bado muda wake wa uongozi haujaisha vinginevyo wasubiri kutangazwa kwa uchaguzi  nakutano Mkuu ndio utaamua.

"Hivi karibuni kwenye mkutano wetu wa kawaida wa TFF walizungumza na kusikika viongozi wa timu za Simba na Yanga kuhusu mimi kuendelea kuongoza  lakini niseme tu kwamba muda wangu haujafika mwisho na wala uchaguzi haujatangazwa kama watu wanamtaka Karia  wasubiri uchaguzi utakapotangazwa , lazima katiba tuziheshumu na twende katika utaratibu ambao unakubalika" alisema Karia.


Share To:

Post A Comment: